Zaidi ya wanafunzi 84 kutoka Cluster ya Ruhita/Msambala wamesonga mbele katika hatua inayofuata ya mashindano ya UMISETA 2026 baada ya kufanya vizuri katika mchujo wa michezo mbalimbali uliofanyika ndani ya cluster hiyo.Wanafunzi hao wataiwakilisha cluster hiyo katika michezo tofauti ikiwemo mpira wa miguu, netball, riadha pamoja na mchezo wa karata katika hatua zinazofuata.Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa, jumla ya wanafunzi 40 wamechaguliwa katika mchezo wa mpira wa miguu ikiwemo wavulana 20 na wasichana 20 huku wanafunzi 20 wamechaguliwa kuunda kikosi cha Netball.Aidha, Jumla ya wanariadha 24 wamechaguliwa kushiriki katika mbio za mita 100, 200, 400 na 1500 ambapo kila kundi limejuisha wanariadha watatu wa kiume na watatu wa kike katika kila mbio husika na wachezaji wengine wakichaguliwa kushiriki mchezo wa karata.Cluster ya Ruhita/Msambala inaundwa na shule za Sekondari za Kigoma Grand, Muka, Mubondo, Ruhita na Msambara.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254















Post a Comment