Kiongozi wa Mbio za Mwenge kitaifa, Wazo Michael Mwang’onda akikagua moja ya madarasa yaliyojengwa kupitia mradi wa Barrick-Twiga Future Forward Education Program katika moja ya Shule ya Sekondari Kongwe ya Ulayasi iliyopo Ludewa Mkoani Njombe.
Muonekano wa sehemu ya moja ya madarasa

Kiongozi wa Mbio za Mwege Kitaifa , Wazo Michael Mwang’onda akizungumza baada ya ukaguzi wa mradi huo wa vyumba vya madarasa saba yaliyojengwa kupitia mradi wa Barrick-Twiga Future Forward Education Program katika shule ya Sekondari ya Ulayasi iliyopo Ludewa Mkoani Njombe

Mradi wa elimu unaotekelezwa na kampuni ya Barrick nchini kwa kushirikiana na Serikali unaojulikana kama Barrick-Twiga Future Forward Education Program kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya shule za sekondari unazidi kunufaisha watoto wa kitanzania ambapo mkoani Njombe katika shule ya Ulayasi umefanikisha ujenzi wa madarasa saba ya kisasa na kuwekewa samani kwa gharama ya shilingi milioni 175.
Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi mbele ya viongozi wa mbio za mwenge kitaifa kabla ya kukaguliwa na kuzinduliwa, Mkuu wa shule ya sekondari ya Ulayasi, Hamika Magaya, alisema mradi wa Barrick-Twiga umefanikisha kumaliza kabisa changamoto ya vyumba vya madarasa shuleni hapo kwa sababu kabla ya ujenzi huo wanafunzi wa kidato cha tano walilazimika kutumia madarasa machache yaliyokuwepo hapo awali na kuathiri udahili wa wanafunzi wakihofia upungufu wa madarasa.
Magaya alisema ujenzi wa miundombinu bora ya madarasa ambao ulianza kutekelezwa mwaka Mei mwaka juzi na kukamilika mwezi Agosti mwaka jana utakuwa na matokeo chanya pia kwenye suala la ufaulu wa wanafunzi kwani kutaepusha mrudikano na kurahisisha ufundishaji na ufundishwaji.
"Kufuatia kukamilika kwa madarasa haya 7 kutaifanya shule kuwa na uwezo wa kudahili wanafunzi wengi miaka ijayo kwa kuwa kuna ziada ya madarasa", alisema Magaya.
Akiongea baada ya kukagua na kuridhia kuzindua mradi huo, kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa 2026, Wazo Michael Mwang'onda, aliipongeza Kampuni ya Barrick kwa kushirikiana na Serikali kutekeleza mradi wa kuboresha miundombinu ya sekondari za Serikali hatua ambayo itawezesha wanafunzi kusoma katika mazingira bora na kuongeza kiwango cha ufaulu.
Alitoa wito kwa wanafunzi, walimu na viongozi kuendelea kusimamia na kutunza mradi huo ili uje kunufaisha vizazi na vizazi vijavyo huku akihimiza wanafunzi kusoma kwa bidii ili kukidhi haya ya wafadhili na serikali ambao wameendelea kuboresha mazingira ya elimu nchini.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ludewa, Olivanus Paul Thomas alisema mradi huo utafanikisha kuongeza kiwango cha taaluma shuleni hapo na kuwakumbusha wanafunzi jukumu lao la kuisaka elimu kwa nguvu zote ili kuzifikia ndoto zao.
Akiongea kwa niaba ya wanafunzi wa sekondari ya juu ambao ni wanufaika wa miundombinu hiyo, Matrida Damas Kalombo alisema kwa sasa wanasoma katika mazingira rafiki yatakayowawezesha kufaulu vizuri katika masomo yao na kutoa shukrani kwa kampuni ya Barrick kwa kushirikiana na Serikali kufanikisha mradi huo.
Awamu ya kwanza ya mradi huu iliweza kunufaisha shule za sekondari za Serikali nchini kote kupitia ujenzi wa madarasa 396, mabweni 97 na vyoo 600 kwa gharama ya dola milioni 10.
Katika awamu ya pili ya mradi inayoendelea iliyoanza machi 2025 ambayo kwa sasa mradi umefikia asilimia 83 na utanufaisha shule 65 kwa kujenga madarasa 318, mabweni 116 na vyoo 542.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254









Post a Comment