Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa imefanikiwa kukusanya Shilingi bilioni 2.7 sawa na asilimia 85 ya lengo la kukusanya Shilingi bilioni 3.2 kupitia mapato ya ndani kwa mwaka wa fedha 2025/2026.Mafanikio hayo yamepatikana huku ikiwa bado miezi miwili kabla ya kumalizika kwa mwaka wa fedha, hali inayoonesha kuimarika kwa mifumo ya ukusanyaji wa mapato pamoja na usimamizi mzuri wa rasilimali za Halmashauri hiyo.Akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani kilichojadili Taarifa ya Maendeleo ya Kata kwa Robo ya Tatu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Bw. Khalid Khalif, amesema mafanikio hayo yametokana na ushirikiano mzuri kati ya viongozi, watendaji na wananchi katika kuhakikisha mapato ya ndani yanaongezeka.Bw. Khalid amesema Halmashauri imeweka mikakati madhubuti ya kuongeza makusanyo ya mapato kwa mwaka wa fedha 2026/2027 ambapo inatarajia kukusanya zaidi ya Shilingi bilioni 3.8, sawa na ongezeko la asilimia 17 kutoka makusanyo ya mwaka huu wa fedha.Ameeleza kuwa Halmashauri itaendelea kuimarisha kilimo cha zao la kokoa katika ukanda wa Ziwa Nyasa pamoja na zao la kahawa katika maeneo ya milimani, mazao ambayo yanatarajiwa kuongeza mapato ya wananchi na Halmashauri kwa ujumla.Aidha, amesema kupitia Wakala wa Mazao Mchanganyiko (COPRA), Halmashauri inatarajia kupata miche kati ya elfu 50 hadi laki moja ya kokoa kwa ajili ya kugawiwa kwa wananchi, sambamba na ununuzi wa zaidi ya miche milioni moja ya kahawa aina ya Arabica ili kuongeza uzalishaji wa mazao hayo ya kimkakati.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa, Mhe. Stewart Nombo, amewataka wataalamu wa ukusanyaji wa mapato kuendelea kusimamia kikamilifu ukusanyaji huo ili Halmashauri iweze kufikia lengo la asilimia 100 kabla ya kuhitimishwa kwa mwaka wa fedha 2025/2026.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254



Post a Comment