Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba amesema hadi kufikia Mei 2026, jumla ya migodi 289 ya wachimbaji wadogo imepatiwa umeme ikiwemo migodi 18 katika Jimbo la Lupa wilayani Chunya mkoani Mbeya ambayo ni pamoja na migodi ya Singa, Chokaa Moja, Mapogoro, Godima Beston, Matfra, Mwambe Mlimanjiwa, Mamboleo, Mbiwe na Mwaoga mbili.Mhe. Salome ameyasema hayo leo Mei 15, 2026 katika Kikao cha 30 cha Mkutano wa tatu wa Bunge la 13 unaoendelea bungeni jijini Dodoma alipokua akijibu swali la Mbunge wa Lupa, Mhe. Masache Kasaka aliyehoji mpango wa serikali wa kupeleka umeme kwenye maeneo ya wachimbaji wadogo.Aidha Mhe. Salome amesema Serikali kupitia kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) inaendelea na utekelezaji wa mradi wa kupeleka umeme katika maeneo ya wachimbaji wadogo wa madini, mashamba ya kilimo na viwanda katika mikoa yote nchini ambapo mpango uliopo kwa sasa ni kufikisha umeme katika maeneo 308 ya wachimbaji wadogo ifikapo Juni 2027." Serikali kupitia REA itaendelea kupeleka umeme katika migodi midogo midogo iliyosalia ili kuwawezesha wachimbaji wadogo kuunganisha umeme katika migodi yao," Amesema Mhe. Salome.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment