Serikali kupitia Wizara ya Maliasili na Utalii imesema itaendelea kushirikiana na Wananchi katika kutatua na kutafuta suluhu ya kudumu ya changamoto mbalimbali ikiwemo migongano baina ya binadamu na WanyamaporiWaziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Ashatu Kijaji (Mb) ameyasema hayo hii leo Mei 17, 2026, Wilayani Chemba Mkoani Dodoma wakati wa ziara ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (Mb),kwa lengo la kueleza mafanikio ya serikali katika wilaya hiyo pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi.Katika ziara hiyo, Dkt. Kijaji ametumia fursa hiyo kukutana na wakazi wa eneo hilo na kusikiliza changamoto zao, hususan zinazohusu migongano kati ya binadamu na wanyamapori.Aidha, Dkt. Kijaji amewahakikishia wananchi kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao katika ikutatua kero zinazowakabili, ikiwemo migongano baina ya binadamu na wanyamapori.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
















Post a Comment