Na Tonny Alphonce -Misalaba MediaKatika hatua ya kuimarisha uelewa wa jamii kuhusu mabadiliko ya tabianchi, tahadhari za mapema na usalama majini, Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA) kwa kushirikiana na Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) wametangaza rasmi kuanzishwa kwa Tuzo za Waandishi wa Habari zitakazolenga kuhamasisha utoaji wa taarifa sahihi na zenye manufaa kwa jamii.Taarifa hiyo limetolewa leo tarehe 28/05/2026 wakati wa mkutano na waandishi wa habari uliofanyika katika ukumbi wa Mbezi Garden jijini Dar es Salaam, ambapo wadau mbalimbali wa sekta ya habari na mazingira walikutana kujadili umuhimu wa vyombo vya habari katika kuelimisha wananchi kuhusu changamoto za hali ya hewa na usalama kwenye maji.Akizungumza katika mkutano huo, Afisa Uchechemuzi kutoka EMEDO, Bi. Mary Francis Mahemba, alisema kuwa waandishi wa habari wana nafasi kubwa katika kuokoa maisha ya wananchi kupitia utoaji wa taarifa sahihi na za wakati kuhusu tahadhari za hali ya hewa pamoja na hatua za kujikinga dhidi ya majanga.“Vyombo vya habari vina mchango mkubwa katika kuijengea jamii uelewa kuhusu hatari zinazoweza kujitokeza kutokana na hali mbaya ya hewa pamoja na ajali zinazotokana na kuzama maji. Kupitia tuzo hizi tunatambua mchango wa waandishi wa habari katika kujenga jamii salama,” alisema Bi. Mahemba.Kwa mujibu wa waandaaji, tuzo hizo zinalenga kuhamasisha utayarishaji wa habari bora zinazogusa maeneo mbalimbali ikiwemo matukio ya hali mbaya ya hewa, tahadhari za mapema, usalama wa vyombo vya usafiri majini, uzuiaji wa ajali za kuzama maji pamoja na ustahimilivu wa jamii dhidi ya majanga yanayochangiwa na mabadiliko ya tabianchi.Tuzo hizo zitawahusisha waandishi wa habari kutoka redio, televisheni, magazeti, mitandao ya kijamii na majukwaa mbalimbali ya kidijitali nchini Tanzania.Waandishi wa habari wametakiwa kuwasilisha kazi zao zilizochapishwa au kurushwa hewani ndani ya kipindi cha kuanzia Agosti 1, 2025 hadi Agosti 30, 2026 kupitia barua pepe media@meteo.go.tz au mediahaliyahewa@gmail.comKwa upande wake, Meneja Masoko na Uhusiano wa TMA, Bi. Monica Mutoni, alisisitiza umuhimu wa matumizi ya taarifa za hali ya hewa na mifumo ya tahadhari za mapema katika kulinda maisha ya wananchi, hasa wale wanaotegemea shughuli za majini kama uvuvi na usafiri wa majini.Uzinduzi wa tuzo hizo unaonekana kuwa hatua muhimu katika kuhamasisha uandishi wa habari wenye tija kwa jamii, huku ukichochea uwajibikaji wa pamoja katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi na majanga yanayohusiana na hali ya hewa.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment