" VIKUNDI 17 KASULU MJI VYANUFAIKA NA MKOPO ASILIMIA 10, ZAIDI YA MILIONI 214 ZATOLEWA

VIKUNDI 17 KASULU MJI VYANUFAIKA NA MKOPO ASILIMIA 10, ZAIDI YA MILIONI 214 ZATOLEWA


Halmashauri ya Mji Kasulu imetoa mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 214 kwa vikundi 17 vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu kupitia mpango wa Serikali wa mikopo ya asilimia 10  ikiwa ni sehemu ya kuwawezesha wananchi kiuchumi.Hafla ya kukabidhi mikopo hiyo imefanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ikiwa ni utekelezaji wa robo ya tatu ya mwaka wa fedha.Akizungumza katika hafla hiyo, Mgeni Rasmi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Kasulu Mjini Prof. Joyce Ndalichako  amewataka wanufaika kutumia fedha hizo kwa ufanisi, uadilifu na kuhakikisha wanazirejesha kwa wakati ili ziweze kuwasaidia wananchi wengine.Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu Sabinus L. Chaula, amesema Halmashauri itaendelea kuunga mkono juhudi za Serikali katika kuwawezesha wananchi kiuchumi kupitia mikopo hiyo.Akifafanua mchanganuo wa fedha hizo, Mkuu wa Divisheni ya Maendeleo ya Jamii  Nurfus Aziz amesema zaidi ya shilingi milioni 113 zimetokana na mapato ya ndani huku zaidi ya milioni 101 zikiwa ni marejesho ya mikopo. Aidha, amebainisha kuwa vikundi nane vya wanawake vimepata zaidi ya milioni 102, vikundi sita vya vijana zaidi ya milioni 101 na vikundi vitatu vya watu wenye ulemavu zaidi ya milioni 10.Naye Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Minza Edward amewataka wanufaika hao kuendelea kuwa mabalozi wa kuwahamasisha watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa ya mikopo hiyo.Baadhi ya wanufaika wa mikopo hiyo wameeleza kuwa watahakikisha wanatumia fedha walizopatiwa kwa malengo yaliyokusudiwa ili kukuza shughuli zao za kiuchumi kwa maendeleo endelevu.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post