Katibu Tawala wa Wilaya ya Kasulu, Theresia Mtewele amewataka viongozi wa Kata ya Murubona kwa kushirikiana na viongozi wa Soko la Sofya kuendelea kuwahamasisha wafanyabiashara kushiriki kikamilifu katika shughuli za usafi ili kuhakikisha soko hilo pamoja na maeneo yanayolizunguka yanakuwa safi na salama wakati wote.Mtewele ametoa wito huo baada ya kushiriki zoezi la usafi katika Soko la Sofya lililopo kata ya Murubona Halmashauri ya Mji Kasulu huku akisisitiza kuwa usafi ni msingi wa afya bora, ustawi wa jamii na maendeleo endelevu.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Ayubu Ngalaba Kilugu amewasisitiza wananchi wote kufanya usafi ili kuepuka hatua za kutozwa faini.Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Mwl. Vumilia Julius Simbeye, amewataka wafanyabiashara kuhakikisha maeneo yao ya biashara yana safi wakati wote ili kujikinga na milipuko ya magonjwa.Akitoa neno la shukrani, Mtendaji wa Kata ya Murubona, Peres Buchanyi ameahidi kuyatekeleza maelekezo yaliyotolewa na viongozi hao kwa kushirikiana na wafanyabiashara na wananchi wa kata hiyo ili kuhakikisha mazingira yanaendelea kuwa safi na yenye kuvutia.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254












Post a Comment