" Wajasiriamali nchini wajumuishwa kwenye Tuzo za Mwajiri bora 2026 (EYA)

Wajasiriamali nchini wajumuishwa kwenye Tuzo za Mwajiri bora 2026 (EYA)


Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania  (ATE) Bi. Suzanne Ndomba – Doran akizungumza na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2026 kwenye ofisi za chama hicho jana jijini Dar es Salaam.Na Damas Makangale , Dar es Salaam, CHAMA cha Waajiri Tanzania (ATE) kwa mara ya kwanza imeijumuisha sekta isiyo rasmi wafanyabiashara wa kati na wadogo (SMEs) na wajasiriamali kwenye tuzo za Mwajiri Bora wa mwaka (EYA) katika juhudi za kutambua mchango kwenye sekta ya ajira na biashara nchini.Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwenye  kwenye uzinduzi rasmi wa Tuzo za Mwajiri bora wa mwaka 2026 , Mtendaji Mkuu wa (ATE) Bi. Suzanne Ndomba – Doran amesema kwamba sekta hiyo ambayo sio rasmi inatatambuliwa kwa juhudi zao katika ustawi wa wafanyakazi, ubunifu wa maadili kazi na mchango wao kwa jamii.“Lakini zaidi ya hapo, tumeifanya hatua kubwa zaidi kwa kuwaunganisha sekta hii ya wajasiriamali ili kuweza kuwatambua juhudi zao na hii ni hatua kubwa kuelekea Tanzania yenye ajira jumuishi zaidi kwa maslahi mapana ya nchini,” amesema Bi Suzanne Ndomba- DoranAliongeza kwamba kwa zaidi ya miongo miwili takribani miaka 20 mpango huo wa kipekee wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) umekuwa nguzo muhimu katika sekta ya ajira na biashara na kuchochea ukuaji wa ajira , usalama mahali pa kazi na ushindani wenye tija hapa nchini. Bi Ndomba – Doran alisisitiza kwamba pamoja na mambo mengine EYA imekuwa si jukwaa la kusherehekea mafaniko bali pia ni kioo kinachoonesha jinsi taasisi mbalimbali zinavyothamini wafanyakazi kwa kuangalia ustawi wao.“EYA imekuwa ikitambua mashirika ambayo hayaangalii faida pekee, bali yanachagua kuwekeza katika wafanyakazi wao, kujenga mazingira bora ya kazi, na kuendesha biashara kwa uwajibikaji na maadili,” Aliongeza .Aliongeza kwamba tuzo za mwajiri bora mwaka 2026 zimekuja na mfumo mpya wa tathimini zaidi ya awali ya rasiliamali watu ila wataanza kuangalia mfumo mzima wa mwajiri bora kwenye maeneo ya uongozi, utawala na mikakati.Bi Ndomba- Doran amesema maeneo mengine ya tathimini ni utamaduni wa shirika , uzoefu wa mfanyakazi , usawa, hai na ujumuishaji, usimamizi wa vipaji na chapa ya mwajiri.Maeneo mengine ni uendelevu wa mazingira , mafunzo na maendeleo, ubunifu na matumizi ya teknolojia katika rasiliamali watu , afya na ustawi wa wafanyakazi , usalama mahali pa kazi na tija , ubora na ubunifu. “Ndiyo maana mwaka huu, kwa mara ya kwanza kabisa, tunaanzisha tuzo za kisekta.sasa kila shirika litashindana ndani ya sekta yake na hii inaleta haki, uhalisia, na ushindani wenye maana zaidi,” amesema Bi Ndomba-Doran.Pamoja na mambo mengine , Mtendaji Mkuu wa ATE alifafanua kwamba chama hicho kimeaanda dawati maalum la kuwasaidia washiriki kujaza madodoso kwenye tovuti kwa njia ya mtandao kwa sababu tuzo za 2026 zitajazwa kwa njia ya mtandao ambayo ni njia rahisi zaidi.“kutambua EYA kama chapa ya kipekee inayostahili hadhi yake kama vile kuanzishwa kwa tovuti maalum ya EYA,”“kuanzishwa kwa tuzo za kisekta, Kutumia wataalamu na wakaguzi wenye weledi na uaminifu, Kuboresha sana vigezo vya tathmini na haya yote yametupa mwelekeo mpya na wenye nguvu zaidi,” Aliongeza.Kwa upande Mtaalamu Mkaguzi kutoka Auditax International , Dkt Straton Makundi amesema kwamba tuzo za mwaka 2026 ni za kipekee kwa sababu washiriki watatumia mfumo mpya wa kidigitali kwa kuingia kwenye tovuti rasmi ya EYA.“Faida za kutumia mfumo wa kidigitali ni kwa muda mfupi washiriki wanaweza kujaza na ni rahisi kuweka kwa ushawishi wa shughuli na viashiria na jinsi unavyotekeleza kwa vitendo vigezo mbalimbali ,” alifafanua Dkt Makundi Mtendaji Mkuu wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi  Suzanne Domba- Doran  akizungumza na waandishi wa habari kwenye uzinduzi wa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2026 , kushoto ni Mtaalamu Mkaguzi kutoka Auditax International , Dkt Straton MakundiMkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE) Bi Joyce Nangai akizungumza kwenye mkutano huo wa uzinduzi wa Tuzo za Mwajiri Bora wa Mwaka 2026 kwenye ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam jana Baadhi ya wafanyakazi wa Chama Cha Waajiri Tanzania (ATE)

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post