Mafunzo ya wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa Vituo vya Kupigia Kura katika Jimbo la Kasulu Mjini yameanza rasmi Mei 29, 2026 yakilenga kuwaimarisha katika utekelezaji wa majukumu yao kuelekea uchaguzi mdogo wa Diwani Kata ya Nyumbigwa.Mafunzo hayo yanafanyika katika Ukumbi wa Fatina Laay uliopo Halmashauri ya Mji Kasulu ambapo Msimamizi wa Uchaguzi wa Jimbo la Kasulu Mjini, Nurfus Aziz Ndee amewasisitiza washiriki wote kutokuwa chanzo cha migogoro badala yake wafanye kazi kwa weledi, uadilifu na ushirikiano na mawakala wa vyama vya siasa vinavyoshiriki ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na uwazi.Mada mbalimbali zitawasilishwa ikiwemo mafunzo kuhusu majukumu ya wasimamizi na wasimamizi wasaidizi wa vituo vya kupigia kura, taratibu za upigaji kura, ufunguaji na ufungaji wa vituo, matumizi sahihi ya vifaa vya uchaguzi pamoja na namna ya kuhesabu kura baada ya uchaguzi.Mafunzo hayo yanafanyika kwa siku mbili kuanzia Mei 29 hadi 30, 2026 ambapo uchaguzi utafanyika tarehe 1 Juni 2026.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment