NA SHEILA KATIKULA-MWANZA WAUMINI wa dini ya Kiislamu nchini wameaswa kutumia kipindi cha Sikukuu ya Eid al-Adha kuwasaidia watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu na hatarishi, ikiwa ni sehemu ya kuendeleza ibada, huruma na mshikamano wa kijamii.Rai hiyo ilitolewa na Sheikh Nouh Mousa wa Jumuiya ya Istiqaama Mwanza wakati wa kukabidhi msaada wa chakula katika vituo vya kulelea watoto yatima vya SOS na Jumuiya ya Ummu Salama vilivyopo jijini Mwanza.Sheikh Mousa alikuwa akizungumza kwa niaba ya kundi la Fatma Sefu, Shamsa Ghania na Ally Salim waliotoa swadaka hiyo kwa lengo la kuwafariji watoto yatima na wenye mahitaji maalumu ili waweze kusherehekea Eid al-Adha kwa furaha sawa na watoto wengine wenye familia.Amesema msaada huo ni ishara ya upendo na kujali jamii, huku akiwataka waumini wengine kuendelea kuwasaidia wahitaji hasa katika kipindi cha sikukuu.“Swadaka hii tumetoa kwa ajili ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu ili nao wajisikie kuthaminiwa na jamii pamoja na kufurahia Sikukuu ya Eid al-Adha kama watoto wengine,” amesema Sheikh Mousa.Kwa upande wake, Msimamizi wa Kituo cha Jumuiya ya Ummu Salama kilichopo eneo la Nera jijini Mwanza, Khadija Omari, amewashukuru wadau hao kwa msaada walioutoa na kuwataka kuendelea kuwakumbuka watoto yatima kila wanapopata fursa ya kutoa sadaka.Naye Kaimu Meneja wa Mradi wa SOS, Uriel Kinuma, akizungumza pamoja na mlezi wa kituo hicho Sheila Mohamedi, wamesema msaada uliotolewa unajumuisha mchele, kondoo, maji na vinywaji baridi bila kutaja gharama kwakuwa kwani itakuwa muendelezo Kwa vituo vingine.Wamesema zaidi ya watoto yatima na wanaoishi katika mazingira magumu 200 wamenunufaika na msaada huo wakati wa maadhimisho ya Sikukuu ya Eid al-Adha.Wamesema kuwa watu wengine Wenye uwezo Kwa mtu Moja Mmoja ama taasisi kubwa mashirika ya asas pamoja na yale ya kiserikali wanapaswa kujitoa kusaidia makundi haya kwakuwa ni Sehemu ya jamii hapa nchini.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment