Na Tonny Alphonce -Misalaba Media Wavuvi 559 wa Wilaya ya Musoma wanatarajiwa kunufaika na mafunzo maalum ya usalama majini ndani ya wiki mbili zijazo, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kupunguza ajali na vifo vitokanavyo na kuzama katika Ziwa Victoria. Mafunzo hayo yanaendelea kufanyika katika Kijiji cha Busekera, moja ya maeneo makubwa ya shughuli za uvuvi wilayani humo, ambapo zaidi ya wavuvi 2,000 hufanya kazi zao za uvuvi kila siku.Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mafunzo hayo, Meneja wa Mradi wa Kuzuia Kuzama Majini kutoka Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) , Arthur Mugema, amesema walengwa wa mafunzo hayo ni pamoja na wavuvi, waegesha mashua na wasindikaji wa samaki, ambao watapatiwa elimu kupitia mradi wa kuzuia kuzama majini unaotekelezwa katika eneo hilo.Mafunzo hayo yanalenga kuwajengea washiriki uwezo wa kujikinga na hatari za majini kwa kuwapatia maarifa kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya uokoaji, stadi za kuogelea, mbinu za usalama wanapokuwa majini pamoja na hatua za kuchukua wakati wa dharura.Mkurugenzi wa Shirika la EMEDO, Bi. Editrudith Lukanga, amesema lengo kuu la mpango huo ni kupunguza na hatimaye kuondoa matukio ya vifo na ajali za kuzama majini. Aidha, amewataka washiriki kutumia elimu hiyo kama mabalozi kwa kuwafikishia wenzao maarifa watakayoyapata ili kuongeza usalama katika maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Musoma na Ziwa Victoria kwa ujumla.Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mafunzo hayo, Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, Kelvin Ruge Gencheere, amependekeza washiriki kupewa vyeti maalum vitakavyowatambulisha rasmi kama wahamasishaji na wakufunzi wa usalama wa majini. Amesema hatua hiyo itasaidia kuunda mtandao wa mabalozi wa usalama watakaosaidia kuendelea kutoa elimu kwa wavuvi wengine.Mafunzo hayo yanatekelezwa na Shirika la EMEDO kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali zikiwemo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Chuo cha Marine Police College na FETA. Akizungumza kwa niaba ya taasisi hizo, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Mwanza, ACF Elisa Mugisha, amesisitiza kuwa elimu hiyo ni muhimu kwa mazingira yote ya majini ndani na nje ya Tanzania, huku washiriki wakiahidi kuitumia na kuisambaza kwa wengine ili kusaidia kupunguza ajali na vifo vinavyotokana na kuzama majini.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment