" BULIGE FC YASHIKA NAFASI YA TATU BAADA YA KUIFUNGA DUARA FC KWA PENATI

BULIGE FC YASHIKA NAFASI YA TATU BAADA YA KUIFUNGA DUARA FC KWA PENATI

Na Mapuli Kitina Misalaba

Timu ya Bulige FC imefanikiwa kumaliza katika nafasi ya tatu ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa mikwaju ya penati dhidi ya Duara FC katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu uliochezwa leo Juni 23, 2026 katika Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.

Ndani ya dakika 90 za mchezo huo, timu zote mbili zilishindwa kufungana na kufanya mchezo kumalizika kwa sare ya bila kufungana.

Matokeo hayo yalipelekea timu hizo kwenda kwenye mikwaju ya penalti ambapo Bulige FC ilionyesha utulivu mkubwa na kufanikiwa kushinda kwa penalti 3-1, ushindi ulioihakikishia nafasi ya tatu katika mashindano hayo.

Kwa ushindi huo, Bulige FC imeondoka na zawadi ya mshindi wa tatu, huku Duara FC ikimaliza mashindano hayo katika nafasi ya nne baada ya kuonyesha ushindani mkubwa tangu kuanza kwa michuano hiyo.

Macho ya mashabiki sasa yanaelekezwa katika mchezo wa fainali utakaowakutanisha Ufukunyungu FC kutoka Manispaa ya Shinyanga na Kashishi FC kutoka Kata ya Solwa, mchezo utakaoamua bingwa wa NIACHEKONA CUP 2026.

Mashindano hayo yameandaliwa na Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation, yakilenga kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha mshikamano wa jamii.

Kwa huduma za MC, matangazo na ushereheshaji wa matukio mbalimbali, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.

 

 

Post a Comment

Previous Post Next Post