Kamishna wa Polisi Jamii (CP) Alex Mkama amewataka askari wanaotekeleza majukumu ya Polisi Jamii kwenda sambamba na mabadiliko ya wakati kwa kutumia mbinu bunifu zitakazosaidia kukabiliana na changamoto zinazoendelea kujitokeza katika jamii.CP Mkama ametoa wito huo wakati akizungumza na Polisi Kata kutoka wilaya za Kishapu na Shinyanga, Askari wa Dawati la Jinsia na Watoto pamoja na askari kutoka vikosi mbalimbali katika ukumbi wa Bwalo la Polisi Manispaa ya Shinyanga.CP Mkama, amesisitiza umuhimu wa kuimarisha utekelezaji wa miradi ya Polisi Jamii kwa kuzingatia mahitaji ya sasa ya wananchi ili kuongeza ushirikiano kati ya Jeshi la Polisi na jamii katika kudumisha amani na usalama.Aidha, amewahimiza askari hao kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuzingatia misingi ya taaluma, uadilifu na uwajibikaji, huku akisisitiza mapambano dhidi ya vitendo vya rushwa vinavyoweza kudhoofisha imani ya wananchi kwa Jeshi la Polisi.Vilevile, ameeleza kuwa ni muhimu kwa askari kutambua vihatarishi vinavyoweza kuathiri usalama wa jamii mapema, ikiwemo migogoro ya kijamii, ukatili wa kijinsia, uhalifu wa watoto pamoja na matishio mengine ya kiusalama, ili hatua stahiki ziweze kuchukuliwa kwa wakati.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254





Post a Comment