Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Umoja wa Wazazi Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ally Salum Hapi, akiwa mkoani Shinyanga, amesisitiza umuhimu wa vyama vya siasa kuendeleza siasa za amani, hoja na maendeleo kwa maslahi ya wananchi.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara, Hapi amesema kuwa baada ya kurejea kwa shughuli za kisiasa za baadhi ya viongozi wa upinzani, wananchi wanatarajia kusikia mawazo, sera na mikakati yenye kuleta maendeleo na kutatua changamoto zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku.
Amesema kuwa katika mazingira ya demokrasia yenye amani, ushindani wa kisiasa unapaswa kujengwa katika misingi ya kuheshimiana, kuwasilisha hoja mbadala na kutoa suluhisho kwa changamoto za wananchi, badala ya kuendeleza migongano na malumbano yasiyo na tija kwa ustawi wa taifa.
Hapi amesisitiza kuwa amani, umoja na mshikamano wa Watanzania ni nguzo muhimu zinazowezesha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, hivyo viongozi na wanachama wa vyama vyote vya siasa wanapaswa kuendelea kuhubiri utulivu na kujenga mazingira yanayokuza maelewano nchini.
Aidha, amewahimiza wananchi wa Shinyanga kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo na kudumisha amani, huku akiipongeza Serikali ya CCM chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan kwa juhudi zake za kuimarisha huduma za kijamii na kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo nchini
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


.jpeg)

Post a Comment