Mwenyekiti wa Kamati ya Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026, Silas Elias Kadaso, amewaalika wananchi, wadau wa michezo na wapenda soka kujitokeza kwa wingi kushuhudia fainali ya mashindano hayo itakayofanyika Jumanne, Juni 23, 2026 katika Uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Akizungumza baada ya kukamilika kwa michezo ya nusu fainali, Kadaso amesema siku hiyo kutachezwa michezo miwili muhimu, ambapo kuanzia saa nane mchana Duara FC itamenyana na Bulige FC katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu.
Baada ya mchezo huo, kutafuata shughuli mbalimbali zikiwemo burudani na hotuba ya mgeni rasmi, kabla ya kuanza kwa pambano kubwa la fainali litakalowakutanisha Ufukunyungu FC kutoka Mjini Shinyanga na Kashishi FC kutoka Kata ya Solwa, timu ambazo zimefuzu hatua hiyo baada ya kufanya vizuri katika michezo ya nusu fainali.
Kadaso amesema mshindi wa kwanza wa mashindano hayo atazawadiwa shilingi milioni moja na laki mbili (1,200,000), huku mshindi wa pili akipata shilingi laki sita (600,000) na mshindi wa tatu akiondoka na shilingi laki tatu (300,000).
Aidha, amesema kutakuwa na zawadi maalum kwa washindi wa tuzo mbalimbali, zikiwemo mfungaji bora, mchezaji bora, golikipa bora pamoja na timu yenye nidhamu zaidi, ambapo kila mshindi atapatiwa shilingi elfu 50,000.
Ameongeza kuwa maandalizi ya fainali yanaendelea vizuri na kwamba kesho kutatolewa taarifa rasmi kuhusu mgeni rasmi atakayehudhuria na kuzindua shughuli za siku ya fainali.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa na Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation, yakilenga kuibua vipaji vya vijana, kukuza michezo na kuimarisha mshikamano wa jamii.
Kwa huduma za MC, matangazo na ushereheshaji wa matukio mbalimbali, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia namba 0757 267 738.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment