Kuelekea mchezo wa fainali ya NIACHEKONA CUP 2026
utakaopigwa leo Juni 23, 2026 katika Uwanja wa Mwabenda, kocha na mashabiki wa Kashishi
FC wameonyesha kujiamini na kueleza kuwa timu yao ipo tayari kwa pambano dhidi
ya Ufukunyungu FC.
Wakizungumza na Misalaba Media kwa nyakati tofauti,
wamesema maandalizi yamekamilika na wachezaji wako katika hali nzuri ya
ushindani, huku wakiamini juhudi walizozifanya tangu kuanza kwa mashindano hayo
zitawasaidia kufikia lengo la kutwaa ubingwa.
Mashabiki wa timu hiyo nao wameahidi kujitokeza kwa
wingi kuipa nguvu Kashishi FC, wakieleza kuwa wana imani kubwa na kikosi chao
kuelekea mchezo huo wa maamuzi.
Leo macho yote yataelekezwa katika pambano hilo
litakaloamua bingwa mpya wa NIACHEKONA CUP 2026, huku maelfu ya mashabiki
wakitarajiwa kujitokeza kushuhudia mchezo huo.
Mashindano hayo yameandaliwa na Paul Daud Augustino
(MC NIACHEKONA) kwa ufadhili wa Shirika la Lushu Foundation.
Kwa huduma za MC, wasiliana na MC NIACHEKONA kupitia
namba 0757 267 738.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment