" MADEREVA WA PIKIPIKI KAHAMA WAPATIWA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA TAA ZA BARABARANI KUPUNGUZA AJALI

MADEREVA WA PIKIPIKI KAHAMA WAPATIWA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA TAA ZA BARABARANI KUPUNGUZA AJALI


 Madereva wa pikipiki katika Manispaa ya Kahama wamepatiwa elimu kuhusu matumizi sahihi ya taa za kuongozea magari barabarani, katika juhudi za kupunguza ajali zinazoweza kuepukika.


Elimu hiyo imetolewa na Askari wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kahama, Koplo Zuhura Mlungwana, katika eneo la Barabara ya Lumambo.

Koplo Mlungwana amewasisitiza madereva hao kuzingatia Sheria za Usalama Barabarani kwa kufuata ipasavyo maelekezo ya taa pamoja na alama nyingine za usalama barabarani bila kusukumwa.

Aidha, amewataka madereva wa pikipiki kuepuka kubeba mizigo inayozidi uwezo wa vyombo vyao vya usafiri, akieleza kuwa hali hiyo inaweza kusababisha kupoteza mwelekeo na hatimaye ajali.

Kwa upande wao, madereva wa pikipiki wameahidi kuzingatia elimu hiyo kwa kufuata sheria za usalama barabarani na kuwa mabalozi wazuri wa kuhamasisha wengine kutumia barabara kwa usalama wakati wote.

Post a Comment

Previous Post Next Post