MWANDISHI WETU, DODOMAMwenyekiti wa Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa, Mary Chatanda, ameshiriki kikamilifu bonanza la CRDB Bank Grand Bunge 2026, Jijini Dodoma.Bonanza hilo la aina yake la kukata na shoka, limefanyika Juni 20, 2026, ambapo matembezi ya pamoja yalianzia viwanja vya Bunge kuelekea uwanja wa Jamhuri. "Bonanza hili linatuleta pamoja viongozi, wafanyakazi na wananchi. Michezo ni afya na inajenga mahusiano mema, hivyo naipongeza benki ya CRDB na uongozi wa bunge kwa kuratibu bonanza hili la aina yake," amesema Chatanda.Sambamba na hilo, Chatanda amesema mazoezi na michezo ni kinga dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza, hivyo ni muhimu kwa wananchi kushiriki michezo."Wahenga walisema kinga ni bora kuliko tiba, miili yetu inahitaji mazoezi ili kuwa imara zaidi dhidi ya magonjwa yasiyoambukiza, binafsi napenda kufanya mazoezi na ninawashauri Watanzania wenzangu kufanya mazoezi," amesema.Kadhalika, bonanza hilo lilichagizwa na kaulimbiu isemayo "Pamoja AFCON 2027, Tanzania Tupo Tayari," ikiwa ni hamasa ya utayari wa Tanzania kuandaa mashindano ya AFCON hapo mwakani.Aidha, bonanza lilipambwa na wadau wengi wakiwemo mawaziri, wabunge, mabalozi, Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, wafanyakazi wa CRDB na wa serikalini, pamoja na wananchi, huku Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Daniel Sillo akiwa Mgeni Rasmi.Baadhi ya washiriki wamepongeza bonanza hilo, kwani limeimarisha afya zao na kujenga mahusiano mema ya kijamii, ambayo yanahitajika katika jamii na katika ujenzi wa Taifa.Bonanza hilo limehusisha matembezi ya pamoja, mpira wa miguu, mchezo wa bao, pool table na kukimbia kwa viatu vya matairi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254




Post a Comment