" MEXICO YATINGA HATUA YA MTOANO KOMBE LA DUNIA 2026

MEXICO YATINGA HATUA YA MTOANO KOMBE LA DUNIA 2026


Timu ya Taifa ya Mexico imefuzu hatua ya mtoano ya michuano ya Kombe la Dunia 2026 baada ya kukusanya pointi 6 kutokana na ushindi katika michezo yake miwili ya awali, huku ikiwa imebakiza mechi moja ya mwisho ya Kundi A. Mexico ilithibitisha kufuzu baada ya kuifunga Korea Kusini mabao 1-0.

Katika msimamo wa Kundi A, Mexico inaongoza kwa pointi 6, ikifuatiwa na Korea Kusini yenye pointi 3, huku Czechia na Afrika Kusini zikiwa na pointi 1 kila moja.

Katika michezo ya mwisho ya Kundi A itakayochezwa Juni 24, Korea Kusini itavaana na Afrika Kusini, huku Mexico ikimenyana na Czechia.

Post a Comment

Previous Post Next Post