Na Mapuli Kitina Misalaba
Timu ya Shilabela FC imefanikiwa kutinga hatua
inayofuata ya mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 baada ya kuibuka na ushindi wa
mabao 3-0 dhidi ya Lyabukande FC katika mchezo uliochezwa leo Juni 3, 2026 kwenye
uwanja wa Mwabenda, Kata ya Solwa, Halmashauri ya Wilaya ya Shinyanga.
Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kwanza kati ya timu
hizo, Shilabela FC iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Lyabukande FC.
Hivyo, kwa matokeo ya leo ya mabao 3-0, Shilabela FC imefanikiwa kusonga mbele
kwa jumla ya mabao 4-0 katika michezo yote miwili. Ushindi huo umeihakikishia
Shilabela FC nafasi ya kutinga hatua ya timu 12 bora za mashindano ya
NIACHEKONA CUP 2026.
Kwa matokeo hayo, safari ya Lyabukande FC katika
mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 imefikia tamati baada ya kushindwa kuhimili
presha ya wapinzani wao Shilabela FC walioonesha kiwango kizuri mbele ya
mashabiki waliojitokeza kwa wingi kushuhudia pambano hilo.
Akizungumza baada ya mchezo huo, Makamu Mwenyekiti wa
mashindano ya NIACHEKONA CUP, Samwel Stephen, ametangaza kuwa mchezo unaofuata
utachezwa kesho ambapo Kashishi FC itamenyana na Kimandaguli FC katika pambano
linalotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Ameendelea kuwakaribisha wananchi, wadau wa michezo na
mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi katika uwanja wa Mwabenda ili kuendelea
kushuhudia vipaji vya vijana na burudani ya michezo inayotolewa kupitia
mashindano hayo.
Mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yameandaliwa
na mdau wa michezo Paul Daud Augustino maarufu MC NIACHEKONA kwa
ufadhili wa shirika la Lushu Foundation, yakiwa na lengo la kuibua vipaji vya
vijana, kuimarisha amani na kukuza michezo katika jamii.
Kwa mawasiliano ya huduma za ushereheshaji wa shughuli
mbalimbali, matangazo na matukio ya kijamii, MC NIACHEKONA anapatikana
kupitia namba 0757 267 738.
Wachezaji wa Shilabela FC na Lyabukande FC wakioneshana ushindani mkubwa katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanayoendelea kwenye uwanja wa Mwabenda.
Wachezaji wa Shilabela FC na Lyabukande FC wakioneshana ushindani mkubwa katika mashindano ya NIACHEKONA CUP 2026 yanayoendelea kwenye uwanja wa Mwabenda.
Wachezaji wa Shilabela FC wakishangilia moja ya mabao matatu yaliyoipa ushindi dhidi ya Lyabukande FC.
Viongozi wa mashindano na wadau wa michezo wakifuatilia mchezo wa Shilabela FC dhidi ya Lyabukande FC.
Mashabiki wa soka wakifuatilia kwa hamasa kubwa mchezo kati ya Shilabela FC na Lyabukande FC katika uwanja wa Mwabenda.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment