" VIJANA DAR ES SALAAM, WATAKA YA OKTOBA 29, KUWA SOMO LA KUTAMBUA UMUHIMU WA AMANI

VIJANA DAR ES SALAAM, WATAKA YA OKTOBA 29, KUWA SOMO LA KUTAMBUA UMUHIMU WA AMANI


Vijana wajasiriamali kutoka Mkoa wa Dar es Salaam wametoa msimamo na kusisitiza kuwa kamwe hawataingia tena barabarani kushiriki maandamano yasiyo rasmi yanayohamasishwa kufanyika Julai 07, mwaka huu, msimamo unaokuja kama onyo kwa vikundi vinavyojaribu kuwashawishi vijana kujihusisha na vurugu zinazoweza kuvunja amani ya nchi.
Wakizungumza kwa sauti moja, vijana hao wamebainisha kuwa hawako tayari kutumika kama madaraja ya machafuko ambayo mwisho wa siku yanawaumiza wao wenyewe kiuchumi na kijamii, wakiaisitiza kuwa utatuzi wa kero za wananchi unaofanywa na serikali katika ngazi mbalimbali ni jambo tosha kabisa na linalopaswa kuungwa mkono na kila Mtanzania badala ya kuhamasisha matukio ya kuhatarisha amani ya Tanzania.
"Kila mtu anacho cha kujifunza Oktoba 29, kilichotokea kilimgusa kila mtu. Hatukuwahi na hatupaswi kuwa Nchi ya kufungiana ndani siku mbili au tatu. Naomba tutoe elimu pia kwa Vijana wengine, Oktoba 29 haikuwa siku ya kawaida na jambo lile halipaswi tena kujirudia." Amesema Bw. James Yuster, Mkurugenzi wa Taasisi binafsi ya James Foundation, yenye kusaidia watoto na Vijana wanaoishi katika mazingira magumu Nchini.

Wakati wa mazungumzo Yao hilii leo na Mwandishi wetu wa habari, Vijana hao akiwemo pia Bw. Julian Noah Kayuni, Mkazi wa Makongo juu, wamewataka vijana wote nchini kukumbuka kwa umakini athari kubwa zilizotokea wakati wa machafuko ya Oktoba 29, 2025, wakitaka kumbukumbu hiyo chungu kuwa somo tosha kabla ya mtu yeyote kufanya maamuzi ya kukurupuka na kuingia barabarani bila kufikiria hatari ya mbele.

Msisitizo mkubwa umewekwa kwenye kulinda amani ya nchi ambayo ndiyo nguzo kuu ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla, Vijana hao wakieleza kuwa bila amani hakuna yeyote anayeweza kufanya shughuli zake za kila siku, wakisema ni wajibu wa kila kijana kuwa mlinzi wa amani ya mwenzake ili kulinda mustakabali wa maisha yao na vizazi vijavyo, badala ya kuwa chanzo cha kubomoa nchi.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post