WABUNGE wamepongeza marekebisho yaliyofanywa na serikali katika Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2026 yaliyoleta nafuu kubwa kwa wananchi baada ya serikali kukubali mapendekezo yaliyotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti.
Pia, wameipongeza serikali kwa kusikiliza maoni ya bunge na wadau kwa kuondoa au kurekebisha baadhi ya hatua za kodi zilizokuwa zimezua wasiwasi.
Miongoni mwa mabadiliko yaliyopokelewa kwa furaha zaidi ni kuondolewa kwa ushuru wa bidhaa wa asilimia tano uliopendekezwa kutozwa kwa pikipiki na kufutwa kwa mpango wa kuongeza ada ya usajili wa pikipiki kutoka Sh 95,000 hadi Sh 150,000.
Akichangia, Mbunge wa Mbarali, Bahati Ndingo (CCM) alisema serikali imeonesha usikivu kwa kukubali mapendekezo ya kamati hiyo.
Mbunge wa Ludewa, Joseph Kamonga (CCM) alisema bunge limefanikiwa kuishawishi serikali kuondoa vifungu ambavyo vingewaongezea wananchi mzigo usio wa lazima.
Mbunge wa Viti Maalumu, Dk Pindi Chana (CCM) alipongeza kuondolewa kwa ushuru uliopendekezwa kwa sukari inayozalishwa nchini, akisema hatua hiyo ingeweza kuchochea mfumuko wa bei na kuongeza gharama za vyakula.
“Watanzania ni zaidi ya milioni 64 na karibu kila familia hutumia sukari kila siku. Ongezeko lolote la kodi ya sukari lingeathiri bei za vyakula na bidhaa zinazouzwa na wajasiriamali wadogo,” alisema.
Dk Pindi alipongeza mageuzi yanayoruhusu asilimia tano ya mapato ya ndani ya mamlaka za serikali za mitaa kutengwa kwa ajili ya kuboresha miundombinu inayowawezesha wanawake wafanyabiashara na wajasiriamali.
Kwa mujibu wake, fedha hizo zitasaidia kuboresha masoko, barabara na huduma za usafi, hivyo kuimarisha mazingira ya biashara kwa wanawake.
Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba (CCM) alisema ameridhishwa na utayari wa serikali wa kusikiliza wabunge na kufanya marekebisho ya mapendekezo yaliyozua mjadala.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment