Na Mwandishi Wetu, Arusha
TAASISI ya kupambana na kuzika rushwa (TAKUKURU), Mkoa wa Arusha imefanikiwa kumkamata aliyekuwa mratibu wa mfuko wa Tasaf Jiji la Arusha, Amani Elifatio Mlay aliyekimbia baada ya kuhukumiwa kifungo cha miaka20 jela kufuatia kutiwa hatiani kwa makosa ya matumizi ya nyaraka za uongo na udanganyifu.
Januari 26, 2026 Mahakama ya Wilaya ya Arushawa ilimhukumu Amani Elifatio Mlay kifungo cha miaka20 jela baada ya kumkuta na hatia ya ubadhirifu wa Shilingi Mil 64,200,000 zilizokuwa za ujenzi wa uzio katika shule ya msingi Shangarao.
Akizungumza na waandishi wa habari Leo Juni 24,2026 ofisini kwake, Kamanda wa TAKUKURU Mkoa wa Arusha, Zawadi Ngailo, amesema mshitakiwa huyo alikutwa na hatia tarehe 16 Januari 2026 na Mahakama, baada ya kubainika kuhusika na uwasilishaji wa nyaraka za uongo zilizotumika kumdanganya mwajiri wake katika mnchakato wa utekelezaji wa mradi wa ujenzi wa uzio wa Shule ya Msingi Shangarao.
Kamanda Ngailo amesema kuwa katika mwenendo wa kesi hiyo, Mahakama ilithibitisha kuwa mshitakiwa aliandaa na kuwasilisha nyaraka zilizodai kuwa vifaa vya ujenzi vyenye thamani ya shilingi milioni 64.2 vilikuwa vimepokelewa na kutolewa na mzabuni husika, wakati ukweli ni kwamba hakukuwa na uwasilishaji halisi wa vifaa hivyo.
Amesema baada ya hukumu kutolewa, mshitakiwa alitoroka Mahakamani kabla ya kuanza kutumikia adhabu yake, hali iliyosababisha Mahakama kutoa hati ya kukamatwa kwake ili kuhakikisha anafikishwa katika mkono wa Sheria.
Kamanda Ngailo amesema mshtakiwa huyo aliyetoroka mahakamani katika shauri namba 000011512/2024 katika mahakama ya Wilaya ya Arusha, alikamatwa Mangaka Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara jumapili ya Juni21, 2026
“ Baada ya ufuatiliaji wa kiintelijensia uliofanywa na TAKUKURU, mtuhumiwa alifanikiwa kukamatwa na kurejeshwa mkoani Arusha kwa ajili ya hatua zaidi za kisheria na utekelezaji wa hukumu yake. Tukio hili linaonesha dhamira ya takukuru kuhakikisha kuwa hakuna mtu atakayejificha ili kukwepa mkono wa sheria,” Amesema.
Amesema Takukuru itaendelea kushirikiana na vyombo vingine vya dola katika kupambana na rushwa na uhalifu wa kiuchumi nchini na kutoa wito kwa wananchi kuendelea kutoa taarifa za viashiria vya rushwa na udanganyifu katika miradi ya umma ili kusaidia kulinda rasilimali za taifa na kuhakikisha ziinawanufaisha walengwa waliokusudiwa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment