Na Paul Kayanda, KahamaDIWANI wa Kata ya Majengo, Manispaa ya Kahama Mkoani Shinyanga Zacharia Shida Soko, ameendelea kuandika historia ya utumishi kwa kukabidhi samani za kisasa zenye thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 2.5 kwa Ofisi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Majengo, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi aliyoitoa kwa wananchi.Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo mbele ya Kamati ya Siasa ya Kata iliyoongozwa na Mwenyekiti wa CCM Kata ya Majengo, Noel Mseven, Diwani Soko alisema lengo lake ni kuboresha mazingira ya ofisi hiyo ambayo ni kitovu cha uongozi na maandalizi ya viongozi wa chama.Alisema hatua hiyo ni sehemu ya shukrani zake kwa CCM kwa kuendelea kumuamini na kumpa nafasi ya kuwatumikia wananchi wa Kata ya Majengo.Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Kata ya Majengo, Noel Mseven, alimpongeza Diwani Soko kwa kujitolea kwake, akieleza kuwa mbali na msaada huo wa samani, amekuwa mstari wa mbele katika utoaji wa chakula mashuleni na ukarabati wa miundombinu ya barabara za mitaa, jambo linaloendelea kuleta maendeleo kwa wananchi wa kata hiyo.Hata hivyo akizungumza kwenye makabidhiano ya thamani hizo, katibu wa CCM Kata ya Majengo SeSebastian Masonga alisema thamani hizo ni chachu ya maendeleo kupitia diwani huyo na kuwataka watumisho wa ofisi ya Kata kuzitunza thamani hizo na kuzitumia kwa matumizi ya ofisi kwani diwani anadhamila ya kuwaletea maendeleo.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment