Shirika la Endeleza Wazee Kigoma (EWAKI) limezindua rasmi mradi wa kuimarisha sauti za wazee Wilaya ya Kasulu wenye lengo la kuibua na kutatua changamoto zinazowakabili wazee katika jamii.Uzinduzi huo umefanyika katika Ukumbi wa Fatina H. Laay uliopo Halmashauri hiyo, ambapo wazee wamepata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali na kupatiwa majibu papo kwa papo kutoka kwa wataalamu.Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Naibu Mkurugenzi wa Shirika la Endeleza Wazee Kigoma (EWAKI) Frank Baseka amesema lengo la mradi huo ni kusikiliza na kutafuta suluhisho la changamoto zinazowakabili wazee kwa kuimarisha ushirikiano na Serikali, asasi za kiraia, wadau mbalimbali na wataalamu kutoka Halmashauri.Aidha, ameeleza kuwa mradi huo utaanza kutekelezwa katika kata tisa ambapo wazee watapatiwa elimu kuhusu usalama wa kipato na uchumi, afya pamoja na mapambano dhidi ya ukatili.Kwa upande wake, Afisa Ustawi wa Jamii wa Halmashauri hiyo Festo Poncian Solly amesisitiza umuhimu wa kuanzisha na kuimarisha afua zinazohusika na masuala ya wazee sambamba na kuhakikisha wazee wote wanashirikishwa kikamilifu katika maamuzi ya maendeleo ndani ya familia na jamii kwa ujumla.Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kasulu, Ayubu Ngalaba Kilugu amelipongeza shirika la Endeleza Wazee Kigoma (EWAKI) kwa kuanzisha mradi huo, akiahidi kuwa Halmashauri itaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha ili kuhakikisha wazee wanalindwa, wanatunzwa na wanapewa haki na stahiki zao kwa kuwa ni hazina muhimu ya taifa.Kwa niaba ya washiriki, wazee waliohudhuria uzinduzi huo wameishukuru EWAKI kwa kuanzisha mradi huo wakieleza kuwa utawapa fursa ya kutoa maoni, kueleza changamoto zinazowakabili na kushiriki kikamilifu katika kutafuta suluhisho litakaloboresha ustawi na maisha yao katika jamii.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
















Post a Comment