Watumishi wa Halmashauri ya Mji Kasulu wamekumbushwa kuzingatia matumizi sahihi ya Mfumo wa upimaji wa utendaji kazi wa watumishi wa umma (PEPMIS) katika utekelezaji wa mpango kazi wa kalenda ya mwaka na mwaka mpya wa fedha 2026/2027.Akizungumza katika kikao maalumu, Mkuu wa Divisheni ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Halmashauri hiyo, Nduwayo B. Elias amewasisitiza watumishi wote kuhakikisha wanaandaa na kuingiza taarifa kwa usahihi na kwa kuzingatia mpangilio unaotakiwa ili kuepusha changamoto zinazoweza kujitokeza baadaye.Aidha, amewataka watumishi kuepuka kuweka majukumu yanayoingiliana katika mpango kazi, kwani hali hiyo inaweza kusababisha kupungua kwa alama za tathmini ya utendaji kazi.Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Nurfus Aziz Ndee amewataka watumishi wote kuwasilisha changamoto zote wanazokutana nazo katika matumizi ya Mfumo wa PEPMIS katika Ofisi ya Utumishi na Utawala ili zipatiwe ufumbuzi kwa wakati.Katika hatua nyingine, watumishi wameahidi kutumia mfumo huo kwa ufanisi sambamba na kutekeleza maelekezo yote waliyopewa.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254








Post a Comment