Wabunge wa Mkoa wa Ruvuma wamefanya ziara ya kutembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara ya Lutukira–Songea yenye urefu wa kilomita 100 pamoja na barabara ya mchepuko yenye urefu wa kilomita 16 wenye thamani ya zaidi billion 150Mara baada ya kukagua maendeleo ya mradi huo, wabunge hao walisisitiza umuhimu wa kuzingatiwa kwa haki za wafanyakazi kwa kufuata sheria, kanuni na miongozo ya kazi, sambamba na kuhakikisha utu na usalama wao vinapewa kipaumbele wakati wote wa utekelezaji wa mradi.Walisema kuwa kuzingatia masuala hayo kutachangia kuongeza ufanisi na tija katika utekelezaji wa mradi, huku wakieleza kuwa matarajio yao ni kuona mradi huo unakamilika kwa wakati na kuleta fursa za kiuchumi pamoja na kuboresha maisha ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma.Kwa upande wake, Meneja wa TANROADS Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Saleh Juma, alisema kuwa hadi sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 10, ambapo kazi za awali tayari zimeanza kufanyika katika maeneo mbalimbali.Aidha, Mhandisi Juma alibainisha kuwa TANROADS itaendelea kusimamia kwa karibu utekelezaji wa mradi huo ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati, kwa ubora unaotakiwa na kufikia malengo yaliyowekwa kwa manufaa ya wananchi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254







Post a Comment