Viongozi wa Mkoa wa Ruvuma wametakiwa kuwa sauti ya wananchi kwa kushughulikia changamoto zao na kuwahamasisha kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kuharakisha maendeleo.
Maagizo hayo yalitolewa katika mkutano maalum uliowakutanisha viongozi wa Serikali na Chama Cha Mapinduzi (CCM), uliofanyika katika Ukumbi wa Songea Club, Manispaa ya Songea, mkoani Ruvuma.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas Ahmed, alisema lengo la mkutano huo halikuwa tu kutathmini mafanikio yaliyopatikana, bali pia kutafakari kwa kina namna ya kuongeza kasi ya utekelezaji wa majukumu ya viongozi kwa manufaa ya wananchi.
Alisema ni muhimu kuimarisha uwajibikaji, kuendeleza maadili ya uongozi na kuhakikisha wananchi wanaendelea kunufaika na rasilimali pamoja na fursa zilizopo katika mkoa huo.
Aidha, aliwataka viongozi kuwa mstari wa mbele katika kutatua changamoto za wananchi, kusimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili kuhakikisha thamani ya fedha inaonekana, kuhamasisha wananchi kufanya kazi kwa bidii na kuendelea kulinda maadili ya uongozi.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma, Comrade Oddo Mwisho, alisisitiza umuhimu wa kuwa na ushirikiano mzuri kati ya viongozi wa Chama na Serikali katika ngazi zote.
Pia alieleza umuhimu wa viongozi kupeana taarifa kwa wakati ili kuhakikisha kila mmoja anashiriki kikamilifu katika shughuli na mipango ya maendeleo kwa manufaa ya wananchi.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254


Post a Comment