Wakati tafiti za hivi karibuni zikionesha kuwa matatizo ya afya ya akili yameongezeka na kufikia takribani asilimia 45, yakizipiku baadhi ya magonjwa yaliyokuwa yakiongoza kwa mzigo wa magonjwa, Wilaya ya Namtumbo imeanza mkakati wa kuwafikia watumishi wa umma, hususan wanawake, kwa kuwapatia elimu ya afya ya akili kupitia Namtugwa Women's Gala, ikiwa ni sehemu ya juhudi za kuimarisha ustawi wa watumishi na kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Namtumbo, Ngollo Ng'waniduhu Malenya, alisema uamuzi wa kuwakutanisha wanawake pamoja na madaktari bingwa wa afya ya akili ulitokana na ongezeko la changamoto za msongo wa mawazo, migogoro ya kifamilia na athari zake katika utendaji wa kazi.
Alisema afya ya akili imekuwa ikichangia kuporomoka kwa tija kazini, kupoteza ajira, migogoro katika jamii na hata vifo, hivyo elimu ndiyo hatua ya kwanza ya kuwasaidia watumishi kujitambua na kutafuta matibabu mapema.
Akitoa mada, Dkt. Roselyne Malenya, Mtaalamu Bingwa wa Saikolojia ya Tiba kutoka Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Afya ya Akili Milembe, alisema afya ya akili huathiri hisia, fikra na tabia za mtu, huku akieleza kuwa sababu kuu za ongezeko la matatizo hayo ni mabadiliko ya kijamii, migogoro ya mahusiano, msongo wa maisha, changamoto za kiuchumi na urithi wa vinasaba. Alisisitiza kuwa wagonjwa wengi huchelewa kufika hospitalini kutokana na kutokuzitambua dalili za awali na hofu ya unyanyapaa.
Kwa upande wake, Dkt. Gavin Kweka kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili alisema afya ya akili ina uhusiano wa moja kwa moja na magonjwa sugu yasiyoambukiza, akieleza kuwa msongo wa mawazo unaweza kujidhihirisha kwa kukosa usingizi, maumivu ya kichwa, kiungulia, kupoteza hamu ya kula au kula kupita kiasi, pamoja na kujitenga na jamii. Aliwataka wanawake kuendelea kuwa nguzo ya utulivu wa familia kwa kujenga mazingira yanayosaidia kudhibiti hisia, fikra na tabia.
Awali akifungua gala hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brigedia Jenerali Ahmed Abbas, aliwataka wanawake kutambua mchango wao katika kujenga jamii yenye afya bora ya akili, akisisitiza kuwa wao ni msingi wa malezi, maadili na maendeleo ya taifa, hivyo elimu waliyoipata inapaswa kuwa mwanzo wa mapambano dhidi ya janga linaloendelea kuathiri familia na jamii.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment