Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amesema Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeendeleza dhamira yake ya kuwekeza zaidi katika huduma za matibabu ya Saratani katika Mfumo wa Fahamu (neuro-oncology) na kuimarisha mfumo wa afya kwa ujumla.

Makamu wa Rais amesema hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Kimataifa wa Watalaam wa Magonjwa ya Saratani katika Mfumo wa Fahamu wa Nchi za Kusini Mwa Jangwa la Sahara (SNOSSA), unaofanyika katika Hoteli ya Johari Rotana, Jijini Dar es Salaam. Amesema Tanzania imeendelea kuimarisha uwezo wa uchunguzi, utoaji matibabu na uimarishaji wa vifaa tiba kuanzia ngazi ya msingi hadi hospitali ya Taifa.

Makamu wa Rais ameongeza kwamba, Tanzania imeendelea kuboresha matibabu ya saratani ambapo kufikia sasa hospitali tatu za kanda na hospitali tatu binafsi zimeanza tiba ya mionzi, zikienda sambamba na Taasisi ya Saratani ya Ocean Road iliyotoa huduma hiyo kwa zaidi ya miaka 30. Pia amesema Serikali imeboresha huduma za Radiolojia na upigaji picha katika hospitali zote za Kitaifa na za kanda, ikienda sambamba na uwekaji wa mashine saba mpya za MRI, na kufanya jumla ya mashine 13 za MRI.

Halikadhalika, Makamu wa Rais amesema Tanzania kama nchi nyingine, bado inakabiliwa na changamoto ya kuongezeka kwa magonjwa ya saratani katika mfumo wa fahamu yanayotokana na mabadiliko ya mtindo wa Maisha, kiharusi, matukio mengi ya majeraha ya ubongo yanayotokana na ajali za barabarani, ambavyo vinazidi mfumo wa huduma ya afya.

Makamu wa Rais ametaja hatua zitakazochukuliwa na Tanzania katika kukabiliana na magonjwa ya saratani katika mfumo wa fahamu ikiwemo kuboresha miundombinu na teknolojia kama vile utoaji wa vifaa tiba vya kisasa, kuimarisha rasilimali watu kwa utoaji wa mafunzo ikilenga kuongeza idadi ya wataalamu bobezi, madaktari bingwa wa neva, madaktari bingwa wa saratani na wengineo.

Vilevile amesema Serikali itaendelea kufadhili bunifu na matumizi ya rasilimali za ndani ili kuboresha upatikanaji na usawa katika utoaji wa huduma ya afya pamoja na kuchagiza utafiti na uvumbuzi. Pia kuimarisha ushirikiano kati ya sekta za umma na binafsi ili kuongeza ufanisi katika matumizi ya rasilimali na utoaji wa huduma katika ngazi zote, kwaajili ya kuhakikisha huduma ya afya kwa wote.

Tanzania kupitia Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) ndio mwenyeji wa mkutano huo, kutokana na uwekezaji mkubwa unaofanywa na serikali katika kuimarisha huduma za afya na vifaa tiba na kuongezeka kwa wataalamu bobezi.

Mkutano huo unawakutanisha wataalamu, watafiti na wadau wa sekta ya afya zaidi ya 200 kutoka ndani na nje ya Afrika kujadili maendeleo ya tiba ya magonjwa ya mfumo wa fahamu hususani saratani za ubongo. Aidha washiriki hao wanajadili kuboresha namna ya upatikanaji wa huduma za afya na kujadiliana baadhi ya mambo yanayofanya kuwe na pengo mkubwa katika utoaji wa huduma zinazowahusu wagonjwa wanaopata saratani katika mfumo wa fahamu.

Mkutano huo unafanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 13-15 Julai 2026.

     SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254