
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu) Mhandisi Felchesmi Mramba (wa kwanza kulia) akisaini kitabu Cha wageni leo, Julai 13, 2026, wakati alipotembelea banda la Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.



Afisa Uhusiano Kampuni ya ETDCO Bi. Samia Chande (wa kwanza kulia) akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu) Mhandisi Felchesmi Mramba wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo katika maonesho ya sabasaba

Maafisa wa Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) wakiwa katika picha ya pamoja katika maonesho ya sabasaba
……..
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati (Umeme na Nishati Jadidifu) Mhandisi Felchesmi Mramba, leo, Julai 13, 2026, ametembelea banda la Kampuni ya Ujenzi na Ukarabati wa Miundombinu ya Usafirishaji na Usambazaji wa Umeme (ETDCO) katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo, Katibu Mkuu alipokelewa na timu ya wataalamu kutoka ETDCO, ambapo alipata fursa ya kujionea utekelezaji wa miradi mbalimbali ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya usafirishaji na usambazaji wa umeme inayotekelezwa na kampuni hiyo katika maeneo mbalimbali nchini.SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment