" NCHI IKO SALAMA, TUTAILINDA KWA WIVU MKUBWA - KATAMBI

NCHI IKO SALAMA, TUTAILINDA KWA WIVU MKUBWA - KATAMBI

 

Na Dotto Kwilasa,Dodoma

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Patrobas Katambi amesema nchi iko salama huku akiwataka wananchi kuendelea na shughuli za maendeleo huku akimshukuru Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa maelekezo na maagizo yake mahsusi katika kuimarisha Ulinzi na Usalama wa nchi.

Ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati wa Ziara ya Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba, leo Julai 17, 2026 ambapo amekagua na kupokea Taarifa ya Maandalizi ya Maadhimisho ya Siku ya Mashujaa yanayotarajiwa kufanyika Julai 25, 2026 katika Viwanja vya Mashujaa, Mtumba,jijini Dodoma.

“Nchi yetu iko salama,ulinzi wa mipaka unaendelea vizuri lakini pia ulinzi dhidi ya Taifa letu dhidi ya mashambulio ya nje yanadhibitiwa vizuri sana na Vyombo vyetu vya Ulinzi na Usalama.

Ulinzi wa ndani ya Nchi ni zingatio letu na kipaumbele chetu muhimu na hivyo tuwahakikishie wananchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wako salama na wageni wanaokuja kwa kufuata utaratibu pia wako salama,majukumu ya uwekezaji lakini pia ujenzi wa uchumi wa Taifa letu tunaulinda kwa wivu mkubwa kama jinsi ambavyo tunarithi wale ambao wamepigania Taifa letu hata kupoteza maisha yao na sisi hivyo tunajifunza.

Tutalilinda Taifa letu tutalitetea na kulipigania ili Tanzania iendelee kubaki salama ikiwa yenye amani na utulivu na maendeleo endelevu kwa ajili ya vizazi.” amesema Waziri Katambi

Post a Comment

Previous Post Next Post