" RC TANGA BALOZI BATILDA BURIAN AMPONGEZA ‘CEO’ WA TARURA KWA UBORA WA BARABARA LUSHOTO

RC TANGA BALOZI BATILDA BURIAN AMPONGEZA ‘CEO’ WA TARURA KWA UBORA WA BARABARA LUSHOTO




Na Tonny Alphonce -Misalaba Media - Dar es Salaam

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Balozi Dkt. Batilda Burian amempongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor Seff kwa usimamizi mzuri wa ujenzi wa barabara ya Wilaya ya Lushoto, akisema mradi huo umeonyesha kiwango cha juu cha ubora kilichotambuliwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru.

Mhe. Balozi Dkt. Batilda ametoa  pongezi hizo wakati alipotembelea banda Jumuishi  la Ofisi ya Waziri Mkuu na Taasisi zake katika Maonesho ya 50 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba), ambapo alipatiwa maelezo kuhusu shughuli mbalimbali na mafanikio ya TARURA.

Akizungumza baada ya kupokea maelezo hayo, Mkuu wa Mkoa huyo alisema ujumbe wake wa shukrani na pongezi ufikishwe kwa Mtendaji Mkuu wa TARURA kutokana na utekelezaji wa mradi huo wa barabara ya Lushoto uliotembelewa na Mwenge wa Uhuru mwaka huu.


Alisema baada ya Mwenge wa Uhuru kufanya ukaguzi na tathmini ya barabara hiyo, viongozi wa Mwenge waliridhishwa  na ubora wa kazi iliyofanyika.

"Baada ya Mwenge kuipima barabara hiyo waliridhika kwa ubora wake na kuchukua Sampuli ya lami (core) kwenda nayo kama mfano wa ubora wa ujenzi wa barabara," alisema

Alieleza kuwa mafanikio hayo yanaonesha umuhimu wa usimamizi madhubuti, utaalamu na uzingatiaji wa viwango katika utekelezaji wa miradi ya miundombinu nchini.

 SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment

Previous Post Next Post