" SIMBA DAY 2026 KUFANYIKA UWANJA WA UHURU AGOSTI 8, SHAMLA SHAMLA ZAANZA

SIMBA DAY 2026 KUFANYIKA UWANJA WA UHURU AGOSTI 8, SHAMLA SHAMLA ZAANZA


 Klabu ya Simba imetangaza kuwa kilele cha tamasha la Simba Day 2026 kitafanyika Agosti 8, 2026 katika Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam, huku kikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 90 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo.

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally, amesema hayo leo Jumatano Julai 22, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, ambapo amesema awali walikuwa na matarajio ya kufanyia tamasha hilo katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kutokana na ukubwa wa tukio hilo, lakini uwanja huo upo kwenye matengenezo.

“Simba Day 2026 itafanyika kwenye Uwanja wa Uhuru. Kutokana na ukubwa wa tamasha hili duniani tunatamani kufanyika kwenye Uwanja wa Mkapa, lakini kwa sasa upo kwenye matengenezo hivyo uwanja ambao utatumika ni Uwanja wa Uhuru,” amesema Ahmed.

Ameongeza kuwa tamasha hilo litakuwa la kipekee kwa kuwa litakwenda sambamba na kumbukumbu ya miaka 90 ya Simba Sports Club, huku mashabiki wakitarajiwa kushiriki katika matukio mbalimbali ya kuadhimisha historia ya klabu hiyo.

SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254.

Post a Comment

Previous Post Next Post