" TEKNOLOJIA ILIYOPO KWENYE SEKTA YA MADINI KUCHOCHEA UKUAJI

TEKNOLOJIA ILIYOPO KWENYE SEKTA YA MADINI KUCHOCHEA UKUAJI



Wadau wa sekta ya madini nchini wamedhamiria kuongeza jitihada ili waweze kuinuka kiuchumi kutokana na uwepo wa madini mengi katika maeneo tofauti hapa Tanzania vilevile kuwepo kwa teknolojia za kisasa.


Wakizungumza leo jijini Mwanza katika maonesho ya Jukwaa la tano la ushirikishwaji wa Watanzania katika sekta ya madini walisema umefika wakati kwa watanzania kutumia sekta ya madini kuinuka kiuchumi.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Geomine ServiceLtd, Geofrey William alisema kampuni yao ambayo inafanya shughuli za utafiti kwa wachimbaji wadogo, kati na wakubwa inaona kuwepo kwa fursa ya haraka kwa wachimbaji kukuwa kiuchumi hapa nchini kutokana na kuwepo kwa mazingira rafiki.

Alisema kutokana na shughuli hiyo kuwa ni ya gharama kubwa huhamasisha wachimbaji wadogo kuungana kwenye vikundi vyenye leseni zao na hivyo huwafikia kwa ajili ya kuwasaidia kubaini maeneo yenye madini ili wachimbe.

Post a Comment

Previous Post Next Post