" SMAUJATA YAHAMASISHA JAMII KUENZI NA KUHIFADHI UTAMADUNI

SMAUJATA YAHAMASISHA JAMII KUENZI NA KUHIFADHI UTAMADUNI

Wananchi nchini wamehimizwa kuendelea kuthamini, kuenzi na kuhifadhi utamaduni wa Kitanzania ili kuendeleza maadili mema, kuimarisha umoja wa kitaifa na kuchochea maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Wito huo umetolewa na viongozi wa Idara ya Utamaduni, Makongamano na Utalii ya SMAUJATA, (Mkurugenzi wa Idara hiyo taifa Shujaa Hashim Omary na Mwenyekiti wa Idara hiyo kanda ya ziwa Shujaa Daniel Kapaya) wakati wakitembelea utalii katika makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere, viongozi hao wameeleza kuwa utamaduni ni urithi muhimu unaotambulisha historia, mila, desturi na utambulisho wa taifa. Wamesema kizazi cha sasa kina wajibu wa kuhakikisha urithi huo unatunzwa na kurithishwa kwa vizazi vijavyo.

Aidha, wameeleza kuwa utamaduni unaweza kuwa chanzo kikubwa cha maendeleo kupitia sekta ya utalii wa ndani na nje, sanaa, michezo ya asili, mavazi ya jadi, vyakula vya asili na kazi za mikono, ambazo huchangia kuongeza kipato kwa wananchi na kukuza uchumi wa nchi.

Viongozi hao wamewataka wazazi, walimu na viongozi wa jamii kushirikiana kuwalea watoto katika misingi ya maadili mema na kuwafundisha historia pamoja na mila zinazojenga mshikamano na uzalendo, huku wakikemea mila na desturi zinazochochea ukatili, ubaguzi au kukiuka haki za binadamu.

Pia wamewahimiza wananchi kutembelea maeneo ya kihistoria na makumbusho yaliyopo nchini ili kujifunza historia ya Tanzania na kutambua mchango wa viongozi waliopigania uhuru, umoja na maendeleo ya taifa.

Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wameeleza kuwa kuenzi utamaduni kutasaidia vijana kujitambua, kujivunia utaifa wao na kujiepusha na mienendo inayoweza kuathiri maadili ya jamii.

SMAUJATA imeahidi kuendelea kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali katika kuhamasisha uhifadhi wa utamaduni, kuendeleza elimu ya maadili na kuhimiza matumizi ya urithi wa kitamaduni kama nyenzo ya kujenga taifa lenye umoja, amani na maendeleo endelevu.


SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

 

Post a Comment

Previous Post Next Post