NA: MWANDISHI WETU
Rai imetolewa kwa wadau mbalimbali kujitoa kwa hali na mali kuchangia fedha kwa ajili ya mfuko unaohudumia wagonjwa wa figo na upandikizaji uloto kwa watoto wenye selimundu (sickle cell) wanaopatiwa matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa (BMH) ya jijini Dodoma.
Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti Taifa wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT), Mary Chatanda, Julai 13, 2026, jijini Dodoma.
Chatanda amesema, kutokana na gharama kubwa za matibabu ya magonjwa hayo, viongozi, taasisi binafsi, asasi za kiraia na wananchi kwa ujumla hawana budi kuunganisha nguvu ya pamoja, kuwezesha upatikanaji wa shilingi bilioni saba, ili wagonjwa wasio na uwezo, waweze kunufaika na mfuko huo na hatimaye kuokoa maisha yao.
"Wenzetu Hospitali ya Benjamin Mkapa, wamekuja na mpango kabambe wa kukusanya shilingi bilioni saba za kugharamia wagonjwa wa figo na selimundu, na UWT tuliposhirikishwa tuliona ni jambo jema kwani linagusa uhai wa watu, hivyo basi, niwaombe wadau na wananchi kwa ujumla kuchangia kuwezesha kuokoa maisha ya wagonjwa hao," amesema Chatanda.
Aidha, amesema upatikanaji wa fedha hizo utawezesha kuleta matumaini ya wagonjwa hao kuishi tena na ndiyo maana hafla hiyo imepewa jina la "Okoa Maisha Gala".
"Hata jina la tukio hili linajieleza wazi, yaani Okoa Maisha Gala, na sisi UWT tuko sambamba na serikali yetu ambayo imewekeza fedha nyingi katika uboreshaji wa sekta ya afya ili kuokoa maisha ya wananchi kwani wananchi wanapokuwa na afya njema, wanakuwa na uwezo wa kufanya shughuli zao za kujiingizia kipato na kujenga uchumi wa nchi," ameongeza.
Katika kuadhimisha miaka kumi ya utoaji huduma, BMH wameratibu hafla ya uchangiaji ili kupata fedha za kutibu wagonjwa wa figo na selimundu. Hafla hiyo inatarajiwa kuongozwa na Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, Julai 16, 2026, katika Ukumbi wa Mabeyo wa jijini Dodoma.
SHY TALENT FILMS - CONTENT YA MWISHO DRAMA
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment