" TANESCO RUVUMA YACHUKUA TAHADHARI KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO

TANESCO RUVUMA YACHUKUA TAHADHARI KUKABILIANA NA MVUA ZA EL NIÑO

 


Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mkoa wa Ruvuma limeanza kuchukua hatua za tahadhari kukabiliana na athari zinazoweza kusababishwa na mvua za El Niño, ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya umeme katika maeneo hatarishi na kutoa elimu ya usalama kwa wananchi.

Akizungumza katika mahojiano maalum na kituo cha redio mkoani Ruvuma, Afisa Uhusiano na Huduma kwa Wateja wa TANESCO, Allen Njilo, amesema tayari shirika limeanza kubaini maeneo hatarishi, hususan mabondeni na maeneo yenye maji, na limejipanga kuweka nguzo za zege ili kuimarisha miundombinu na kupunguza athari zinazoweza kujitokeza wakati wa mvua.

Kwa upande wake, Mhandisi wa TANESCO, Malibe Boniphace, amesema suala la usalama limepewa kipaumbele kwa kutambua maeneo hatarishi na kuweka mikakati ya kuyakinga. Aidha, amewataka wananchi kutoa taarifa mapema kuhusu miundombinu ya umeme iliyo katika hali hatarishi ili hatua za haraka ziweze kuchukuliwa kabla ya kusababisha madhara zaidi.

TANESCO imeeleza kuwa katika kipindi cha maboresho na matengenezo ya miundombinu, baadhi ya maeneo yanaweza kukumbwa na kukatika umeme kwa muda, hatua inayolenga kuimarisha mfumo na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya umeme kwa uhakika zaidi wakati wa msimu wa mvua.


Aidha, wananchi wametakiwa kutogusa nyaya za umeme zilizoanguka au miundombinu iliyoharibika, bali kutoa taarifa mara moja kwa TANESCO. Shirika hilo limesisitiza kuwa ushirikiano wa wananchi ni muhimu katika kuhakikisha usalama wa watu na mali pamoja na kupunguza madhara yanayoweza kusababishwa na mvua za El Niño

🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA

  • Wasiliana nasi:
    📍 East African Spirits (T) Ltd
    📞 +255 767 650 806 | +255 652

Post a Comment

Previous Post Next Post