Wito umetolewa kwa vijana nchini kuzingatia amani na usalama ili mabilioni ya shilingi yanayotolewa na serikali kupitia mikopo na miradi ya uwezeshaji kiuchumi yaweze kuwanufaisha katika kujiletea maendeleo.
Hayo yameelezwa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, Wazo Mwang’onda, wakati Mwenge ulipotembelea kikundi cha Umoja wa Madereva wa Bodaboda Makere katika Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, akisisitiza kuwa amani na usalama vikiwa mashakani hakuna kijana atakayefaidika na fedha zinazotolewa na serikali.
Mwang'onda amebainisha kuwa serikali imetenga shilingi bilioni mia mbili kwa ajili ya kuinua shughuli za kiuchumi za vijana, huku ikihimiza halmashauri kutumia mapato ya ndani kuwezesha makundi hayo pamoja na wanawake na watu wenye ulemavu, akitolea mfano Halmashauri ya Wilaya ya Kasulu kwa kutoa zaidi ya shilingi bilioni moja kwa mpango huo kwa mwaka uliopita.
Ameongeza kuwa serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imejipambanua katika kuhakikisha vijana wanapata nafasi za uongozi na kuimarishwa kiuchumi ili waweze kujiajiri na kuajiri wenzao kwa maslahi ya taifa.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kikundi cha Madereva Bodaboda Makere, George Kagoma, ameeleza kuwa tangu kuanzishwa kwa kikundi hicho mwaka 2018 wamekopeshwa shilingi milioni sabini nukta tano kutoka mapato ya ndani ya halmashauri, na wanatarajia kumaliza mkopo uliosalia ili kuomba mkopo mwingine wa kununua basi la abiria kwa ajili ya kuimarisha shughuli zao.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
Post a Comment