Watu watatu wanadaiwa kujeruhiwa kwenye maeneo ya miili yao ikiwemo kichwani, mgongoni pamoja na kuvunjwa miguu kwa madai ya kuvamiwa kwenye vurugu kati ya wafugaji wa kabila la maasi na watatoga, mgogoro unaodaiwa unatokana na kugombea maji pamoja na malisho.
Mgogoro huo unahusisha watatoga kutoka Kata ya Eyasi pamoja na Maasai kutoka Kata ya Kakesio zote zimo kwenye tarafa ya Ngorongoro wilayani.
Akizungumza akiwa amelazwa kwenye moja ya hospitali iliyopo eneo la Njiro jijini Arusha, majeruhi wa tukio hilo anasema watu walio mjeruhi walimvamia nyumbani kwake usiku kisha kumpiga na kumjeruhi vibaya na kutoweka na Ng'ombe zaidi ya ishirini pamoja na silaha za jadi.
Majeruhi anaongeza kuwa watu hao walikuwa kwenye kundi kubwa na lengo lilikuwa ni kumuua na baada ya kuwajeruhi vibaya walihisi kuwa wamemuua lakini kumbe alikuwa bado yu hai.
Mashuda wa tukio hilo wanasema hali ya uhasama kati ya makundi hayo inaongezeka siku hadi siku wakiomba hatua za haraka zichukuliwe kumaliza mgogoro huo
Siku kadhaa zilizo pita mgogoro huo uliibuka kwenye kijiji cha Kakesio wakati wafugaji hao walipo pishana kauli wakowa kwenye visima vya asili ndipo kukazuka kwa mgogoro wa kugomea maji
Hali ambayo ilimlazimu mkuu wa mkoa wa Arusha Cpa Amos Makalla kuunda kamati ya viongozi wa mila waliyopewa jukumu la kumaliza mgogoro huo kama ambayo ilifanya kazi hiyo na kufanikisha kuyakutanisha makundi hayo na kufikia mahafaka wa kumaliza mgogoro ambapo kila upande ulitoka Ng'ombe kuchinja kunywa na kula nyama pamoja ikiwa ni ishara ya kumaliza mgogoro ambao hivi karibuni umeeanza tena
Alipoulizwa mkuu wa wilaya ya Ngorongoro kuhusu Taarifa hiyo alisema yupo kwenye eneo ambalo hawezi kuzungumza kwa sasa lakini juhudi zaidi ya kuwatafuta viongozi wa wilaya na mkoa kupata undani wa mgogoro huo zinaendelea.
PROFESSOR MGOKO EP 07
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254

Post a Comment