Na Lydia Lugakila- Misalaba Media
MBEYA
Mchungaji Aron Mwaigwisya, Mkuu wa Idara ya Elimu ya Vyuo vya Biblia wa Pentecostal Holiness Mission (PHM), amesisitiza umuhimu wa kanisa kuhakikisha watumishi wa Mungu wanapata elimu ya kutosha ya Neno la Mungu kabla ya kutumwa kwenda kufanya huduma mbalimbali.
Amesema kuwa elimu ya Neno la Mungu ni msingi muhimu unaomsaidia mtumishi kuelewa wajibu wake, kuwa na uelewa mpana wa mafundisho ya Biblia na kutekeleza huduma kwa ufanisi.
Mwaigwisya alitoa kauli hiyo katika mahafali ya 24 ya PHM Bible College Mbeya yaliyofanyika Novemba 12, 2026, jijini Mbeya, ambapo aliwataka wahitimu kutumia elimu waliyoipata kuwa chachu ya kuimarisha huduma katika maeneo watakayokwenda kulitumikia Kanisa
Amesisitiza kuwa watumishi wanapaswa kuwa na maarifa sahihi ya Neno la Mungu ili waweze kusimamia misingi ya imani na kuwa vielelezo bora kwa jamii wanazozihudumia.
Hata hivyo, amewataka wahitimu kutambua kuwa kuhitimu masomo si mwisho wa kujifunza, bali ni mwanzo wa safari ya kutekeleza kile walichofundishwa na kuendelea kujijengea maarifa katika huduma ya Mungu.
🥃🍶 TUMIA VINYWAJI BORA VYA KAMPUNI YA EAST AFRICAN SPIRITS – BEI RAFIKI, LADHA SAFI BILA HARUFU MBAYA
Wasiliana nasi:
📍 East African Spirits (T) Ltd
📞 +255 767 650 806 | +255 652 096 254
.jpeg)
Post a Comment