" YANGA SC YAICHAPA 4 -0 KAGERA SUGAR

YANGA SC YAICHAPA 4 -0 KAGERA SUGAR

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga wameendelea kukusanya pointi tatu baada ya leo kuifunga Kagera Sugar mabao 4-0 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam.

Mabao ya Yangu yamefungwa na mshambuliaji Peter Shalulile dakika ya 26,
beki wa kushoto wa timu hiyo, Mohamed Hussein ‘Zimbwe JR’, dakika ya 32,
Cheikh Ibrahima dakika ya 88 na 90

Ushindi huo ni wa pili mfululizo kwa Yanga katika Ligi Kuu Bara tangu alipoondoka Manqoba, baada ya mechi iliyopita kushinda mabao 2-1, dhidi ya maafande wa Mashujaa FC, Oktoba 27, 2026, ikiwa chini ya kaimu kocha mkuu kwa sasa, Simo Dladla.

Katika mechi 10, iliyocheza Yanga hadi sasa, imeshinda minane, sare moja na kupoteza pia moja, ikiwa nafasi ya pili na pointi 25, nyuma ya watani zao wa jadi Simba inayoongoza na pointi 27.

Kwa upande wa Kagera iliyocheza 11, imeendeleza mwenendo mbaya hadi sasa, baada ya kushinda mechi moja tu, sare tatu na kupoteza saba, ikiwa mkiani mwa msimamo mwa nafasi ya 16, kufutia kukusanya pointi zake sita.

Post a Comment

Previous Post Next Post