" MWENYEKITI VIWAWA JIMBO LA SHINYANGA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA VIWAWA KANDA YA MWANZA

MWENYEKITI VIWAWA JIMBO LA SHINYANGA ACHAGULIWA KUWA MWENYEKITI WA VIWAWA KANDA YA MWANZA

 Mwenyekiti wa Chama cha Vijana Wakatoliki Wafanyakazi (VIWAWA) wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mwalimu Leonard Mapolu, amechaguliwa kuwa Mwenyekiti wa VIWAWA Metropolitan (kanda) ya Mwanza, inayoundwa na majimbo manane ya Mwanza, Shinyanga, Geita, Bukoba, Musoma, Rulenge-Ngara, Kayanga na Bunda.

Mapolu amechaguliwa kupitia uchaguzi uliofanyika Jumamosi tarehe 22.04.2023. katika Kanisa la Mtakatifu Josephine Bakhita Parokia ya Nyamanoro Jimbo kuu la Mwanza, uliowashirikisha wajumbe kutoka majimbo yote manane yanayounda kanda ya Mwanza, ambao umesimamiwa na Mkurugenzi wa utume wa Walei Jimbo kuu la Mwanza Padre Phabiani Ngeleja, akishirikiana na Mlezi wa Vijana Metropolitan ya Mwanza Padre Emmanuel Lyanga pamoja na Mapadre walezi wa vijana kutoka majimbo yote manane yanayounda Kanda ya Mwanza.
Wengine waliochaguliwa ni Jackson Henerico kutoka Jimbo la Kayanga ambaye amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti wa Kanda, ambapo Musa Masolwa kutoka Jimbo la Geita amechaguliwa kuwa katibu.
halikadhalika Suzana Daud kutoka Jimbo la Shinyanga amechaguliwa kuwa Katibu msaidizi ambapo Ester John kutoka Jimbo la Geita amechaguliwa kuwa Mweka hazina.
Mkutano huo pia umewachagua wajumbe watatu wa kanda ambao ni Gerald Chombo kutoka Jimbo la Geita, Julieth John kutoka Jimbo la Rulenge-Ngara na Otto Kyaruzi kutoka Jimbo la Bukoba.
Kulingana na Katiba ya VIWAWA, Viongozi hao watatumikia nafasi hizo kwa kipindi cha miaka mitatu.

Post a Comment

Previous Post Next Post