Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Halmashauri walei Kanisa kuu la Mama Mwenye Huruma Parokia ya Ngokolo, wamemchagua Ndugu Ignatus Banyemaa kuwa Mwenyekiti mpya wa Parokia hiyo.
Banyemaa ambaye pia ni Mweka hazina wa Kamati ya Mawasiliano Jimbo Katoliki Shinyanga, amechaguliwa kupitia uchaguzi uliofanyika Jumamosi tarehe 22.04.2023, katika ukumbi wa Balina English Medium Primary School, uliopo Ndembezi mjini Shinyanga.
Aidha Bi. Octaviana Kiwone amechaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa Parokia, ambapo Ndugu John Marwa amechaguliwa kwa mara nyingine tena kuwa Mweka hazina wa Parokia hiyo.
Viongozi hao watatumikia nafasi hizo kwa kipindi cha miaka mitatu, kwa mujibu wa Katiba ya Halmashauri Walei.
Post a Comment