" PAROKIA TEULE YA MT. YOSEFU MUME WA BIKRA MARIA NDEMBEZI SHINYANGA YAPATA VIONGOZI WAPYA

PAROKIA TEULE YA MT. YOSEFU MUME WA BIKRA MARIA NDEMBEZI SHINYANGA YAPATA VIONGOZI WAPYA

 Parokia teule ya Mtakatifu Yosefu Mume wa Bikra Maria Ndembezi katika Jimbo Katoliki Shinyanga, imepata viongozi wapya kupitia uchaguzi ulifanyika Jumamosi tarehe 22.04.2023.

Viongozi hao ni Ndugu Victor Ngoya ambaye amechaguliwa kuwa Mwenyekiti ambapo Ndugu Augustino Kisuda amechaguliwa kuwa Makamu Mwenyekiti.
Wengine ni Ndugu Stephen Sabuni ambaye amechaguliwa kuwa Katibu, ambapo Mwalimu Genoveva Luhende amechaguliwa kuwa Katibu Msaidizi.
Aidha wajumbe wa mkutano huo wa uchaguzi wamemchagua Ndugu Brandina George kuwa Mweka hazina wa Parokia hiyo teule.
Parokia teule ya Ndembezi imetangazwa miaka michache iliyopita na Askofu wa Jimbo Katoliki Shinyanga Mhashamu Liberatus Sangu, baada ya kumegwa kwa sehemu ya Parokia ya Mama Mwenye Huruma Ngokolo ili kusogeza huduma za kiroho kwa waamini, ambapo kwa sasa iko kwenye mchakato wa kupewa hadhi ya kuwa Parokia kamili

Post a Comment

Previous Post Next Post