Zoezi kutia saini mikataba ya ujenzi wa miradi ya Maji kwa mwaka wa Fedha 2023/2024  kati ya RUWASA na Wakandarasi/Wazabuni likiendelea.

Na Mapuli Kitina Misalaba 

Jumla ya mikataba  saba ya ujenzi wa miradi ya maji yenye thamani ya zaidi ya shilingi Bilioni 6 Milioni 443  imesainiwa baina ya RUWASA na wakandarasi watakaoitekeleza  katika Mkoa wa  Shinyanga  

Katika hotuba yake kwenye hafla ya utiaji saini wa mikataba hiyo meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi  Julieth Payovera amesema miradi hiyo itatekelezwa katika baadhi ya maeneo ya  Wilaya za Kishapu, Kahama na Shinyanga  

Ameeleza kuwa  mikataba hiyo itatekelezwa katika vijiji 17  kwa muda wa Mwaka mmoja tangu kuanza kwa utekelezaji wake. 

Kipindi cha Mwezi Julai Hadi Disemba Mwaka 2023 RUWASA imeshatangaza jumla ya Zabuni 9 ikihusisha ujenzi miradi 8 na Zabuni moja (1) kwa ajili ya Bomba na vifaa mbalimbali kwa ajili ya ujenzi wa miradi minne (4) itakayotekelezwa kupitia mfumo wa Force Akaunti hadi sasa jumla ya Zabuni saba (7) tayari mchakato wake umekamilika na leo tutashuhudia utiaji saini wa mikataba hiyo na miradi miwili (2) ipo katika hatua za manunuzi”. 

Mikataba tunayosaini leo ni ujenzi wa mradi wa Maji katika vijiji vya Chona, Ubagwe na Bukomela katika Halmashauri ya Ushetu Wilaya ya Kahama Mkandarasi ni Jonta Investment Gharama ya mradi ni Bilioni 1.4 muda wa utekelezaji mradi ni Miezi tisa au siku 270, mkataba wa pili ni ujenzi wa mradi wa maji katika vijiji vya Ng’wampangabule, Zumve, Jimondoli na Sumbigu katika Wilaya ya Shinyanga Mkandarasi ni Otonde Construction and General Supplies mkataba wake ni Bilioni 2.4 muda ni Mwaka mmoja au siku 360, mkataba wa tatu ni ujenzi wa mradi wa Maji katika vijiji vya Ipeja, Itilima, Ikonokelo na Ikoma katika Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu Mkandarasi Corsyne Consult mradi huu tutaanza kwa awamu ya kwanza kwa muda wa Miezi sita(6) au siku 180”. 

“Mkataba wa nne ni ujenzi na upanuzi wa mradi wa Maji Nhobola Wilaya ya Kishapu Mkandarasi ni Geospatial Classic Works utekelezaji wa mradi ni Mienzi sita, mkataba wa tano ni ujenzi wa mradi wa Maji Nyenze – Ng’wanholo kwenda Kabila katika Halmashauri ya Kishapu Mkandarasi ni Geospatial Classic Works utekelezaji wa mradi ni Mienzi sita, mkataba wa sita ni ujenzi na upanuzi wa mradi wa Maji kwenda vijiji vya Wela, Wila, Mwataga na Mwanhulu Wilaya ya Kishapu Mkandarasi ni Geospatial Classic Works utekelezaji wa mradi ni Mienzi sita na mkataba wa mwisho ni  ununuzi wa Bomba la viungo katika vijiji vitano vya Wilaya ya Kahama, Kishapu na Shinyanga Mkandarasi ni Hazglobal Logistics kwa muda wa Mwezi mmoja na nusu au siku 45”.amesema Mhandisi  Julieth Payovera 

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe.Christina Mndeme amesema Mkoa wa Shinyanga umefikia asilimia 66 ya Watu wanaopata huduma ya Maji safi na salama, sawa na wakazi wapatao  milioni 1. Elfu sitini na Nne Mia tano Ishirini na Nne ya wananchi wanaoishi vijijini ambapo amempongeza Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi  Julieth Payovera kwa usimamizi mzuri wa miradi huku akiwataka wakandarasi kutekeleza miradi yao ndani ya muda wa mkataba. 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Mkoa wa Shinyanga Bwana Mabala Mlolwa amesema miradi hiyo ni utekelezaji wa ilani ya chama hicho ambaye naye amemshukuru na kumpongeza meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi  Julieth Payovera kwa kwa kasi na usimamizi mzuri wa miradi ya Maji Mkoani Shinyanga. 

Akizungumza kwa niaba ya Wakandarasi waliosaini mikataba hiyo Mkurugenzi wa kampuni ya GEOSPATIAL Stephen Owawa atakayetekeleza mradi wilayani Kishapu amesema watazingatia ubora wa kazi ukamilishaji kwa wakati uliopangwa. 

Meneja wa RUWASA Mkoa wa Shinyanga Mhandisi  Julieth Payovela akizungumza kwenye hafla hiyo.