Shirika la Usimamizi wa Mazingira na Maendeleo (EMEDO) kupitia mradi wa kuzuia kuzama maji ziwa Victoria Kwa Kushirikiana na Malamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA) wamefunga UBAO WAKIDIGITALI unaopokea na kuonesha taarifa za utabiri wa hali ya hewa kutoka TMA kila siku.
Akizungumza na wakazi wa kisiwa Cha Goziba kilichopo mkoani Kagera, Meneja mradi wa kuzuia kuzama Ziwa Victoria kutoka EMEDO Arthur Mgema amesema Ubao huo (ELECTRONIC WEATHERBOARD) unatumia umeme wa jua unauwezo wa kupokea taarifa ya utabiri wa masaaa 24 yajayo katika ziwa Victoria na kuwataka watumiaji wote waziwa kuangalia ubao huo kabla ya kuingia ziwani Ili kujua hali ya hewa ilivyo Kwa siku husika.
Arthur amewataka wanachi hususani wavuvi wote kuzingatia utabiri unaotolewa na TMA ikiwa ni pamoja na kuvaa maboya okozi wakati wote wanapokuwa kwenye maji sambamba na kumlinda Ubaonhuo wa Utabiri wa Hali ya hewa.
Amesema taarifa za utabiri wa hali ya hewa zimekuwa msaada kwa wakina kwa wafanyabiashara wa dagaa hasawa wanakina mama ambao wanaweza kuangalia hali ya hewa kwa siku ijayo kabla ya kununua dagaa ili kuepusha hasara ambayo wamekuwa wakipata kwa mvua kubyesha mfululizo na kufanya dagaa wasikauke.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa umoja wa wavuvi wilaya ya Muleba Masinde Wengere amewataka wavuvi kuzingatia Usalama wanapokuwa ziwani Kwa kuzingatia Utabiri wa Hali ya hewa na kuvaa Maboya okozi.
"Naomba niwaambie hivi sasa ikitokea mvuvi kafa maji Kwa kutovaa Boya wale wenzie aliokuwanao tutawachikulia hatua Kwa sababu ya uzembe wa kutokumbushana kuvaa Maboya"alisema Wengere
EMEDO imeshafunga mbao zingine tano na kufundisha community weather champions 20 wanaofanya kazi endelevu ya kutoa hamasa na elimu juu ya taarifa za utabiri wahali ya hewa .
Sambamba na shughuli hizo EMEDO kwa kushirikiana na taasisi za serikali zinazohusika na masuala ya usalama kwenye maji wanatarajia kufundisha wavuvi masuaa ya usalama kwenye maji ikiwa pamoja na kujiokoa na kuokoa wengine kupitia program maalumu iliyoandaliwa kwa ushirikiano na wadau.
Post a Comment