" YANGA SC YABEBA KOMBE MBELE YA SIMBA SC 2025

YANGA SC YABEBA KOMBE MBELE YA SIMBA SC 2025




Dakika 90 zimekamilika kwa ubao kusoma Yanga SC 2-0 Simba SC. Ubingwa ukiwa mali ya Yanga SC. Clement Mzize ambaye alianzia benchi kwenye mchezo wa leo amefanya kazi kubwa kipindi cha pili alipoingia kuchukua nafasi ya Prince Dube.

Mabao ya Yanga SC yamefungwa na Pacome dakika ya 66 kwa mkwaju wa penati na Clement Mzize dakika ya 87 akitumia pasi ya Pacome.

Yanga SC imetetea ubingwa wa ligi mbele ya Simba SC. Pointi zao kibindoni ni 82 huku Simba SC nafasi ya pili na pointi 78.

Mchezaji Pacome wa Yanga SC amefikisha mabao 12 ndani ya ligi msimu wa 2024/25 huku Mzize akifikisha mabao 14. Kinara ni Jean Ahoua mwenye mabao 16 na pasi 9 za mabao yeye ni kiungo mshambuliaji wa Simba SC.

Post a Comment

Previous Post Next Post