" PSSSF YAJA NA FARAJA KWA FAMILIA ZA WASTAAFU

PSSSF YAJA NA FARAJA KWA FAMILIA ZA WASTAAFU

Na Mwandishi wetu, Misalaba Media MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umeanza kutoa Fao la Msaada wa Mazishi kwa Wategemezi wa Mstaafu aliyefariki na Fao la Mkupuo wa miezi 36 kwa Wategemezi  wa Mstaafu aliyefariki kwa lengo la kuwashika mkono na kuwapunguzia ukali wa maisha pindi Mpendwa wao anapoondoka.Hayo yamebainishwa leo kwenye maonesho ya Nanenane katika viwanja vya Nyamhongo Jijini Mwanza na Afisa Matekelezo Mkuu Bw. Abdallah Makani alipokuwa akizungumza na wananchi waliofika kwenye banda lao kwa lengo lw kupata elimu ya Hifadhi ya Jamii.Alisema mabadiliko hayo yameanza rasmi Januari mwaka huu ambapo taratibu zote zinafanyika kwa njia ya mtandao ukiwataka walengwa kujaza taarifa zinazotakiwa na hivyo kuwa katika nafasi ya kupata mafao hayo.Makani alisema Fao la Mazishi hutolewa kwa wategemezi wa Mstaafu kwa lengo la kusaidia shughuli za mazishi na fao hili uombwa ndani ya siku 30 baada ya mstaafu kufariki. Aidha, sambamba na fao hilo vilevile kuna mkupuo wa Pensheni ya miezi 36 kwa  Wategemezi wa mstaafu aliyefariki.Makani, alisema malipo yataombwa kwa njia ya mtandao ambapo viambatanisho tajwa vitahitajika kuwepo kuwezesha mchakato huo kukubalika. Mzee mstaafu aliyekuwa Mwalimu katika wilaya ya Magu Mkoani Mwanza, Magembe Saguda (80) alipongeza PSSSF kuanza kutoa huduma hiyo akisema hatua hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wategemezi wa wastaafu waliofariki.Aliomba huduma hiyo kuwa endelevu ili kuwezesha wategemezi wa wastaafu waliofariki kuwa na uhakika wa kumudu maisha yao baada ya kuondokewa na wapendwa wao.

Post a Comment

Previous Post Next Post